Advertisement |
Wakati raia wa nchi kadhaa Barani Afrika wakitamani kwenda nchi za Uarabuni kutafuta ajira, Kituo cha Takwimu cha Saudi Arabia kimetangaza kuwa idadi ya watu wasio na ajira katika nchi hiyo ya Kiarabu imeongezeka.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa idadi ya watu wasio na ajira na wanaotafuta kazi nchini humo imeongezeka na kufikia zaidi ya 1,000,000 na kwamba nusu yao wamehitimu masomo ya Chuo Kikuu.
Taarifa zaidi zinasema kuwa kiwango cha ongezeko la ajira nchini Saudia katika miezi mitatu ya kwanza mwaka huu kilikuwa asilimia 7 huku uchumi wa nchi hiyo ukiripotiwa kuporomoka zaidi.
Makisio ya ripoti hiyo yanaeleza kuwa hadi kufikia mwaka 2030, idadi ya watu wasio na ajira katika nchi ya Saudia itafikia milioni nne na laki moja na kwamba sekta binafsi nchini humo zitatakiwa kuandaa fursa za ajira za idadi hiyo ya watu.
Pia imeelezwa kuwa hali ni mbaya zaidi nchini humo kwani takwimu ambazo zimekuwa zikitolewa na asasi rasmi za serikali ya Saudia kuhusiana na kiwango cha ukosefu wa ajira nchini humo ni kinyume kabisa na ukweli wa mambo.
Licha ya Saudia kuwa na pato la mamia ya mabilioni ya dola kila mwaka kutokana na biashara ya mafuta, takribani asilimia 70 ya wananchi wanaishi katika hali mbaya ya kiuchumi na hawaridhishwi na hali hiyo.
Kutokana na hilo, wananchi wakiongozwa na wanaharakati wanatarajia kufanya maandamano ya kutaka kuweko mabadiliko ya kimsingi katika masuala mbalimbali nchini humo yakiwemo mabadiliko ya kiuchumi.

0 comments: