Sunday, July 30, 2017

Mwiko kumwita Mume kwa jina lake halisi

ad300
Advertisement
Tofauti na ilivyo kwenye maeneo mengi duniani, nchini India mamilioni ya wanawake hawajawai kuwaita waume zao kwa majina yao ikiwa ni njia ya kuonyesha heshima.

Utamaduni huo umetajwa kuheshimika zaidi kwenye maeneo ya vijijini huku mijini  likiwemo jiji la Mumbai kukitajwa kuanza kuuacha utamaduni huo tangu miongo miwili iliyopita.

Sababu ya kupishana huko kumeelezwa kuwa ni mchanganyiko wa utamaduni wa watu mbalimbali ambapo kundi moja la wanaharakati limeibuka na kuanzisha kampeni za kuishauri jamii ya waishio vijijini kuacha utamaduni huo kwani unaondoa usawa.

Kutokana na kampeni hiyo, mwanamke mmoja amejitokeza na kusema Mama yake alioana na Baba yake miaka 73 iliyopita wakati mama yake akiwa na umri wa chini ya miaka 11 na baba alikuwa na miaka 15.

"Katika miaka hiyo yote waliishi pamoja katika kijiji kidogo kwenye jimbo lililo kaskazini mwa India la Uttar Pradesh, mpaka mimi nazaliwa Mama hakuwahi kumuita Baba kwa jina lake hata siku moja.

"Alipokuwa akizungumza na sisi alimuita baba kwa jina "Babuji" ambalo humaanisha "baba" ambalo tulilitumia...alipokuwa akimuita moja kwa moja alitumia jina "Hey ho" linalomanisha wewe," alisema.

Kwenye utamaduni wa India, Mume ni sawa na miungu na kuanzia umri mdogo wanawake hufunzwa kumheshimu.

Inaelezwa kuwa Mwanamke kumwita Mumewe kwa jina lake kunaweza kumletea bahati mbaya na kupunguza maisha yake sambamba na kumsababishia mwanamke husika adhabu kali.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: