Friday, September 1, 2017

Updates baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili EPL na kwingineko

ad300
Advertisement
Saa 6 usiku wa kuamkia Septemba 1, ulikuwa muda rasmi kwa drisha la usajili wa majira ya joto kwenye ligi pendwa ya mpira wa miguu, Ligi ya Uingereza KUFUNGWA!

Kwa wafuatiliaji, tumeona timu zikionyesha jeuri ya fedha kwa 'kuvunja benki zao' ili tu kupata saini ya wachezaji wanaowahitaji kwenye kujihakikishia kikosi bora chenye uwezo wa kutwaa ushindi kwenye mashindano yaliyo mbele yao kwa msimu huu wa 2017/2018.

Licha ya kwamba kulionekana nia, mpaka saa 6 kamili baadhi ya 'deals' hazikufanikiwa kukamilika ikiwemo ya Mamadou Sakho na Danny Drinkwater kwenda Chelsea, japo wengi walitarajia kwenye sekunde za mwisho mambo yangekaa sawa.

Sikatai kuna baadhi ya deals ambazo hufanywa kwa kificho, lakini mwisho wa siku ukweli hubainika hivyo kama hao niliowataja kwa namna yoyote walifanikiwa kumwaga wino kwenye timu zao mpya, basi tutafahamishana.

Adrien Silva amefanikiwa kunaswa na Leicester kwenye dakika za mwisho kabisa akitokea klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno, habari ambazo zimethibitishwa na tovuti rasmi ya klabu hiyo ya nchini Uingereza.

Tottenham waooo, wamewadaka Fernando Llorente na Serge Aurier. 

Ross Barkley kagoma kuondoka Everton licha ya kubembelezwa sana na Chelsea. 

Kilichoshangaza wengi na ambacho kitaendelea kuacha wapenzi wa soka midomo wazi kwa butwaa na issue ya Alexis Sanchez, huwezi kuamini lakini Arsenal wameng'ang'ania mpaka dakika ya mwisho, hivyo HAENDI POPOTE. 

Washika bunduki hao pia, wameshindwa kumpata Thomas Lemar, ambaye Arsene Wenger alionyesha dhahiri kumhitaji kwa udi na uvumba. 

Alex Oxlade-Chamberlain, hii deal ilijulikana mapema sana jana jioni Agosti 31, kwamba kakubali kuitumikia vijogoo vya Anfield, timu ya Liverpool akitokea Arsenal.

Wilfried Bony, karudi nyumbani Swansea baada ya kucheza Manchester City kwa mkopo msimu uliopita. Kuwasili kwake klabuni hapo, anaungana na mgeni mwingine ambaye si mwingine bali Renato Sanches, kinda la Kireno lenye miaka 20 tu aliyewasili kwa mkopo akitokea Bayern Munich.

Kylian Mbappe, kijana aliyesumbua sana vyombo vya habari kwenye usajili huu uliotamatishwa, ameenda kwa mkopo PSG akitokea Monaco, imethibitishwa.


Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: