Thursday, February 20, 2014

TASAF na jitihada za kutokomeza Umasikini uliopitiliza Tanzania

ad300
Advertisement
SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais chini ya mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF), imedhamiria kutokomeza umasikini uliopitiliza ifikapo 2015 ili kutimiza mojawapo ya malengo ya milenia yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa.

Katika kulifanikisha hilo, imeanzisha mpango maalum kwenye awamu ya tatu ya mipango ya taasisi hiyo ya serikali kwa ajili ya kunusuru kaya masikini zilizo katika mazingira hatarishi mpango ambao umezinduliwa na umeanza kufanya kazi.

Akizungumza ofisini kwake Ofisa mawasiliano wa TASAF, Zuhura Mdungi alisema kwakua taasisi hiyo inafanya shughuli zake kwa awamu, mpaka sasa wako katika awamu ya tatu, iliyozinduliwa Agusti, mwaka 2012.

Alisema awamu mbili zilizotangulia zilikuwa zimetoa kipaumbele katika kuboresha huduma za kijamii pamoja na kuwasaidia watu wa makundi maalum wakiwemo walemavu na watoto katika halmashauri zote nchini.

Zuhura alisema awamu waliyopo hivi sasa inatekelezwa kikanda wakizingatia takwimu za umasikini zilizorekodiwa kwenye sensa ya mwaka 2012 ambapo kwa kuanzia halmashauri za Lindi, Mtwara na Tunduma, Unguja na Pemba zinanufaika na mpango huo.

Alisema dhana iliyopo miongoni mwa wananchi kuhusu miradi ya maendeleo inayosimamiwa na TASAF katika maeneo yao kuwa mibovu hivyo kuwatupia lawama ni potofu kwakua wao husimamia utoaji wa fedha kutoka serikali kuu kwenda kwenye maeneo yaliyolengwa na jukumu lililobaki huachiwa Halmashauri husika kupitia waratibu ambao ni wafanyakazi wa halmashauri hiyo.

Aidha alisema kuwa mpango wa sasa unaosimamiwa na TASAF una nia kubwa ya kuondoa umasikini kwakuwa mchakato unafanyika mpaka kupatikana walengwa umezingatia maoni ya wengi, ambao watazibainisha kaya masikini zitakazopatiwa msaada wa kifedha kutoka kwenye Taasisi hiyo kila mwezi huku wakizipa kipaumbele kaya zenye wanawake wajawazito na watoto waliofikia umri wa kwenda shule.

Ofisa huyo alisema mpaka kufikia sasa kaya zaidi ya 40,000 zimenufaika na mpango huo wa kuzinusuru kaya masikini ambapo kaya zaidi zitaendelea kunufaika kwenye kanda zingine ambazo zitafuata baadaye kulingana na takwimu zilizopo za hali ya umasikini kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: