Thursday, April 3, 2014

TCRA yatangaza 'Vita'

ad300
Advertisement
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imejizatiti kudhibiti udanganyifu katika mitandao ya simu za kimataifa nchini kwa kuanza kutumia mitambo maalum ya kusimamia Mawasiliano ya simu na udhibiti wa mapato yatokanayo na simu hizo.

Imeelezwa kuwa Mtambo huo unaojulikana kwa jila la Telecommunication Traffic Monitoring System (TTMS), una uwezo wa kutambua mawasiliano ya udanganyifu katika mitandao pamoja na namba za kitapeli zinazotumika kinyume na matakwa ya sheria na kanuni za udhibiti wa Mawasiliano ya simu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa habari (MAELEZO) jana, Meneja wa Mawasiliano wa TCRA Innocent Mungi alisema kwa kutumia mitambo hiyo na kwa kushirikiana na watoa huduma za Mawasiliano na vyombo vya Usalama wanaimani wataweza kufanikiwa lengo hilo kwa kiasi kikubwa.

Alisema kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia Mamlaka inatambua uwepo wa watu wanaoruhusu simu za kimataifa kuingia nchini bila kupitia njia rasmi, hivyo kuikosesha Serikali mapato kwa mujibu wa Sheria za nchi zinazosimamia Sekta ya Mawasiliano

Mungi alisema TCRA watapambana na watu wa aina hiyo na kuwachukulia hatua za kisheria haraka mara watakapowabaini ili Sekta hiyo iwe salama kwa matumizi ya Wananchi sambamba na Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.

Pia alisema Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye Mawasiliano ya za mkononi kwa kipindi kifupi kutokea watumiaji milioni tatu mwaka 2000 hadi kufikia Milioni 28 kwa Mwaka jana ambapo nchi imeendelea kuboresha huduma hiyo katika upatikanaji na unafuu.

Sambamba na hilo Meneja huyo aliwataka Wananchi watoe ushirikiano kwa Mamlaka hiyo kwa kutoa taarifa haraka endapo watabaini mtu au watu wanaojihusisha na udanganyifu kwa njia za Mtandao. Mpaka sasa Tanzania inakadiriwa kuwa na watumiaji wa huduma za Mtandao 7,600,000.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: