Sunday, September 10, 2017

Simulizi ya Kusisimua, Mateso Yangu Episode 4

ad300
Advertisement
MATESO YANGU –SEHEMU YA NNE 
Mtunzi: Deo Massawe. 0653195298.
Mhariri: William Shechambo.

...Ilipoishia Sehemu ya Tatu

Giza liliingia, Dennis akaingia ndani na kujifungia huku akilia kwa uchungu mambo bibi yake aliyomuelezea yalimfanya aone kama yeye ndo atakayerithi dhambi za baba yake, hivyo akakata tamaa ya kuishi.

***
Haule na Joely walikesha macho wakiuwaza msemo, 'mtoto wa mwenzako sio wako' wakisubiri pakuche.

SASA ENDELEA


Ilikua mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi, siku tatu baada ya marehemu Joseph kuzikwa shughuli ya siku hiyo ilikua kuanua tanga.
Dennis aliamka akiwa na mawazo mengi kwa mambo alioyasikia kuhusu baba yake, hivyo kila alipokua akionana na mtu uso kwa uso, aliumia sana kwa aibu ya kuonekana mtoto wa mtu mnyama uchungu ulizidi pale aliposikia mama mmoja akimkataza mwanaye kuongea na Dennis.

Kwa kweli ilimuuma sana na akaamua kurudi ndani kuwaza ni kwa jinsi gani atayakwepa yote mapema iwezekanavyo.

***
Haule alimkumbusha Joely siku moja alipoenda kuuza mazao ila baada ya kukabiziwa pesa akafuatwa na wale aliowauzia wakamnyang'anya pesa zote hivo wakaamua kutafuta makaratasi mengi wakayaweka kwenye kiroba kisha wakaingia chooni.

Wakatoa pesa kwenye mkoba kisha wakazipanga katikati ya takataka ndani ya kiroba na baadaye wakaelekea kituo cha mabasi lengo lao likiwa ni kupanda gari waende hadi Morogoro mjini kisha waanze shughuli zao maana tayari pesa walikuwa nayo mkononi.

***
Panda panda twende Morogoro... Oyoooo abiria twende twende piga simu waweke uji jikoni utakuta haujachemka wewee.... nauli yako mfuko wa shati Dar es salaam mpaka morogoro elfu 7 yako panda kwenye gari na viatu nyie wanafunzi acheni kuremba panda utoe nusu nauli ukasimame nyuma maana nyie mnaringa sana pandeni mkasome kwa bidii la sivyo hii kazi yangu itawahusu gari yetu leo kwanza ina baraka kwanza inapandwa na wachungaji jamani wapisheni wachungaji wakae siti ya mbele ili wawahi kufika kutangaza injili,"
Yalikua maneno ya utingo mmoja akiwa anapiga debe ndani ya kituo cha mabasi Ubungo tayari kwa safari ya Morogoro ambapo ndani ya gari hilo walipanda akina Joely , Haule pamoja na makamanda wa Filbet ila kwenye hiyo gari walionekana wachungaji wanaoelekea sehemu kufanya maombi ya kufufua watu.

Haule na Joely walikaa siti za mbele kabisa kushoto mwa deveva nae makamanda wa Filbet wakikaa siti ya pili kwa upande wa devera hivo walikaa mgongoni mwa dereva, gari ilijaa na kuondoka.

***

Bi Martha naye alikua katika pilika pilika za kuanua tanga hivo hakua na hata muda wa kuongea na mjukuu wake Dennis hivo naye Dennis  alikaa ndani akiwaza kwa jinsi gani ataweza kujitoa kwenye macho ya watu ili kukwepa aibu ya uchafu wa baba yake ila ghafla likaja wazo la kujiua ila hakujua atajiua kwa namna gani! 

Alijaribu kujinyonga mwenyewe akashangaa hakati roho ila kumbukumbu zikaja akiwa na marehemu baba yake kuna wakati baba alitega panya kwa kutumia sumu kali sana kutoka Zimbabwe na hiyo ilikua na uwezo wa kukatakata utumbo, Dennis akaamini kwa kuwa baba alimwambia nisije kula ule mkate tunaotegea panya nitakufa basi natafuta duka ninunue sumu ya kuua panya nije nile nitakufa na watu hawataniona tena maana nahisi damu baba yangu alizomwaga ndio zinataka kunirudia mimi.

Dennis aliwaza pesa hana ila akakumbuka nje kuna kapu limewekwa kwa ajili ya waombolezaji kuwekea sadaka hivo akapanga kuiba hapo pesa na hapo bila kuchelewa alitoka nje na kuenda moja kwa moja hadi kwenye hilo kapu akazamisha mkono na kutoa noti ya elfu tano kwa wale wachache waliomwona akifanya kile kitendo cha kuchukua pesa hawakusema kitu kutokana na kujua ni mtoto wa nyumbani hivo Dennis alitoka barabarani na kuanza kutafuta duka anunue sumu.

Bi Martha alikua na Furaha kusikia pesa ipo njiani inakuja maana kabla ya Filbet kuwapa ruhusa ya kuondoka mawasiliano yalifanyika kwanza kuhakiki kua washakabiziwa ambapo Haule na Joely walimhakikishia mwenyekiti wa kijiji chao kua tayari washahesabiwa pesa na hiyo ilikua nia ya Filbet kuwapa imani kua ni mtu mwema.

***

Katika barabara ya Dar es salaam kuelekea morogoro basi kulikua na kijana ambae alikua ana kibanda chake cha kuuza karanga hivyo kutokana na kazi yake alipewa jina la Bwana karanga choma licha ya hayo alikua mpole, mstarabu,mnyenyekevu na asiependa ugomvi pia alikua ni mtu anaemwomba sana Mungu na aliishi kwa imani kua siku moja Mungu atayajibu maombi yake ya kuwa tajiri ili aweze kuwapeleka watoto wake shule. 

Kwa hiyo kutokana na huruma yake watu walimuonea sana, kwa kua kibanda chake kilijificha kidogo watu walimtumpia takataka eneo lake lakini hakuchoka kuziokota na kuenda kuzimwaga jalalani hadi watoto wadogo walimcheka sana na kumtania wengine wakimwona huita bwana Katanga choma nae akija hata hawanunui bali yeye huwaonjesha na kuendelea na na safari zake.

***

We konda nyimbo gani hiyo unatuwekea weka nyimbo ya Bony Mwaitege mtoto wa mwenzio muone kama mtoto wako" yalikua maneno ya dada mmoja aliyekerwa na wimbo uilokua ukiimba kwenye gari nae konda akamsihi dereva
Oya suka bonyeza kitu cha Bony Mwaitege hapo kuna dada anataka kukisikiliza huku nyuma" 
"Powa alafu huyo atakua mnyakyusa mwenzake" alisema Dereva huku abiria wengi wakicheka isipokua abiria wanne tu ndani ya gari na nyimbo ilipigwa kila mtu akaifurahia.

***

Dennis alifika dukani ila muuzaji alikua mlevi na hivo hakuweza kuzingatia masharti ya kuuza sumu, akajikuta anauzia mtu anaelia kitu ambacho  nje ya masharti. Dennis alirejea nyumbani huku sumu yake ikiwa  mfukoni, moja kwa moja akanyoosha hadi chumbani na kujifungia.

***

Makamanda wa Filbet walianza harakati za kutafuta namna ya kuanza mpango wa kuua ambapo wao hufanya mawasiliano kwa njia ya ishara na hapo wakapata mbinu ya kusababisha ajali ambapo walipanga kumuua dereva kwa sumu na hapo shughuli ikaanza.

Mmoja alitoa sumu bila abiria yeyote kuona na wakatoa nyuki wao ambapo walimlisha sumu na kisha bila mtu kuona wakamtupa ndani ya nguo za dereva hapo dereva aliumwa na huyo nyuki ambapo kwa kawaida sumu hiyo inaua ndani ya dakika mbili hadi tatu.

Dereva alipata maumivu ya ghafla mgongoni kama amechomwa sindano vile haraka akaingiza mkono na kutoka na nyuki hapo kwa hasira akamtupia mdomoni na kumtafuna kisha kumeza kama mshikaki.

Makamanda wa Filbet walipoona wamefanikiwa kumpa dereva sumu basi wakajua nini kitatokea baada ya muda mfupi hivyo wakamwomba awashushe kituo cha mbele,

"Konda shusha hapo mbele " alisema kamanda wa Filbet,

"Haya sogeeni mlangoni wachungaji halafu naomba uwaombee hawa abiria wangu wanunue magari yao maana wananitesa sana" hapo gari lilifika kituoni na vijana wa Filbet wakashuka na gari likaondoka kwa kasi.

Baada ya makamanda wa Filbet kushuka kwenye gari walijipongeza kwa kwa kuona hatua moja ya kazi imekamilika na ilibaki kupanda gari lingne ili kufika Morogoro kuua waliobaki yaani Denis na bi Martha. 

Walipoangalia saa ya mkononi wakaambizana bado dakika mbili akina Joely wafe kwa hiyo tupande gari tuende zetu na ili tuweze kuona ajali yao. Hapo wakapanda gari na kuondoka.

***

Katika gari waliopanda akina Joely basi kulikua na mlevi alikaa siti ya nyuma mwisho na baada ya gari kuondoka kituo ambacho walishuka makamanda wa Filbet basi mlevi aliongea kwa sauti "Konda nataka kukojoa" konda akamjibu,
"Kojoa" mlevi akamuuliza,
"Vipi konda nikojoe ndani au vipi wewe simamisha gari wewe nikojoe" mlevi aliendelea kulalamika, konda naealizidi kumtania,
"Wewe hiyo pombe uliyokunywa ukafikiri supu?  suka we tembea huyu mlevi tukimpa upenyo wa kukojoa atatuweka masaa hapa" abiria wote walishangillia maana hawakutaka gari lisimame kutokana na watu walitaka kufika waendako haraka na hapo konda aliwasihi abiria waliokaa na mlevi,
“Dada  uliyekaa na huyo ndugu yangu hapo naomba mkalishe vizuri na umfunge mkanda vizuri maana gari ikiruka matuta anaweza tapika pia kaa makini asikojoe huko ndani" abiria walicheka na safari ikaendela lakini haikupita dakika moja konda akatoa sauti kubwa,
"jamaniiiiii abiriaaaa fungeni mk......" hakuweza kumalizia sentensi hiyo.

***

Dennis alikaa ndani akilia huku  sumu yake ikiwa  mkononi akiiombea imuue bila maumivu.
Bi Martha alikua sambamba na shughuli za uandaaji wa kuanua tanga kwa hiyo hakupata mda wa kumliawaza mjuu wake Denis. 

Denis aliwaza kwa jinsi gani atakula sumu bila kitafunio maana alikumbuka hata panya anawekewa kwenye chakula hivo akaamini sumu kavu haitaweza kuua na hapo ndani hakuona chochote cha kuliwa na hapo akaficha sumu yake mfukoni na kusubiria chakula kilichokuepo jikoni.

***

Bwana karanga choma nae siku hiyo alikua amekaa kijiweni kwake bila kuuza kutokana na kutokua na mzigo pesa yote alitumia kuenda kumsaidia mtoto wa kaka yake aliepata ajali na kuumia sana sehemu ya kichwani kutokana na kutovaa kofia ngumu ya kichwani hivyo Bwana karanga choma alikuja kufanya usafi tu kwenye kibanda chake na kurudi nyumbani.

***

Makamanda wa Filbet walifika maeneo ya Kibaha na kukutana na ile ajali ambapo walipochunguza kwa hapo wakagundua kapona mtu mmoja tu na wakafurahi kugundua kwa maelezo walopata haitakua Haule wala Joely. 

Ila kwa kuwa mjini kila mtu anaangalia mambo yake basi wao waliendelea na safari yao wakaacha watu wakiendelea na shughuli ya kuokoa na kuchomoa maiti kwenye gari bila kusahau shughuli za vibaka na mateja pale ajali inapotokea ni kuiba na kusachi majeruhi pamoja na maiti mfukoni.

Sehemu ambapo gari ilipatoa ajali ilikua mita chache kutoka kibanda cha Bwana karanga choma hivo mateja walikua wanaiba mabegi na kuenda kuyafungulia hapo kibandani kwa bwana karanga choma wakiamini hawezi kuwafanya chochote. Kibaka mmoja akasema kwa hasira,

Angalia  hawa wanasafiri na mfuko wana weka takataka ndani washenzi kweli"kiroba kilitupwa huko yaani kati ya siku kibanda cha karanga choma kilichafuliwa ni siku hiyo na ndio alitoka tu kufanye usafi.
***

"Mjukuu wangu kipenzi njoo ule chakula nimekuwekea hapo" bi Martha alimwitia mjukuu wake Dennis chakula hapo Dennis akafurahi kuitiwa kitafunio cha sumu yake,

"Naam bibi nakuja kula niwekee hapo kwenye stuli" Denis alitoka na sumu yake taratibu na akaitia kwenye ndizi nyama zilizoungwa vizuri baada Denis kuichanya sumu bila mtu kuona aliacha chakula sebuleni na kurudi chumbani maana alipata wazo la kuandika kaujumbe ka kuweka wazi kua kajiua mwenyewe akawa anatafuta kalamu chumbani.

***

Makamanda wa Filbet walifuata ramani na tayari walikua kijijini kwa bi Martha kila mtu alitoa salamu kwa heshima,
"Bwana yesu asifiwe ndio salamu iliyoenda nao sambamba na hata bi Martha aliwakaribisha sebuleni,
"Karibuni watumishi wa Mungu kaeni hapa kuna mjukuu wangu pia anaitwa Dennis ambae ndio mtoto wa marehemu anakula hapo kidogo" nao wakaonesha upendo kwa kila mmoja kuchukua ndizi na nyama moja yeye bi Martha akaendelea na shughuli zake ila yote hayo Dennis aliyasikia akiwa chumbani na tayari alishaona kama kuna kitu kitatokea mda mfupi ujao maana tayari chakula chake chenye sumu kishaliwa na watu wengine tena wawili.Makamanda wa Filbert walifanya kula kidogo ili iwe rahisi kukiweka sumu bila kuhisiwa ila kumbe wao tayari washakula sumu na Dennis bado hajatokea.
Je nini kitatokea ? Tukutane tena hapa hapa siku chache zijazo.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: