Thursday, February 20, 2014

Kisutu waiburuza DAWASCO Mahakamani

ad300
Advertisement
MAMLAKA ya maji safi na maji taka DAWASCO, imeburuzwa mahakamani kutokana na kushindwa kurekebisha miundombinu inayoisimamia kwenye soko la kimataifa la Kisutu jijini Dar es Salaam hali inayochangia kushusha hadhi ya soko hilo.

Hilo limekuja baada ya Mamlaka hiyo kukiri kushindwa kurekebisha mtandao wa maji machafu unaopita katikati ya soko hilo ambapo chemba mojawapo imefurika na kumwaga maji machafu kwenye eneo la soko.

Kwa nyakati tofauti wafanyabiashara katika soko hilo waliozungumza na blog hii, walisema chemba hiyo ya maji machafu inalotapika uchafu kwa siku kadhaa sasa hali inayohatarisha afya za wafanyabiashara, wapitanjia na wateja kwa ujumla.

Walisema wamefanya juhudi kadhaa kulitatua tatizo hilo ikiwemo kutoa taarifa kwa uongozi wa soko ili waweze kupata ufumbuzi mara viongozi hao watakapolipeleka katika ngazi za juu za serikali.

Katibu mkuu wa soko la Kisutu, Suitbert Nyawale ameliambia Uhuru kuwa taarifa hizo amezipata na kuwa ameripoti kwa afisa afya wa Kata aliyechukua hatua ya kuwaarifu DAWASCO wakitarajia ufumbuzi wa tatizo hilo haraka.

Nyawale alisema tofauti na matarajio wafanyakazi wa DAWASCO walitembelea eneo hilo mara kadhaa na kukiri kuwa wameshindwa kulitatua kwakua unahitajika utaalamu zaidi ili kuweza kurudisha chemba hiyo katika hali ya kawaida.

Alisema walifanya juhudi zaidi wakishirikiana na Halmashauri ya manispaa ya Ilala na Ofisa Afya wa Kata ambao walikubaliana kulipeleka suala hilo kwenye mikono ya sheria ambapo waliishitaki DAWASCO kwa kushindwa kutimiza wajibu wao kwa manufaa ya jamii.

Chemba hiyo imeendelea kutoa maji machafu kwenye eneo kubwa la soko hilo, hali inayohatarisha afya za binadamu kutokana na uwezekano wa kutokea magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: