Friday, September 1, 2017

Simulizi ya Kusisimua - Mateso yangu Sehemu ya Kwanza

ad300
Advertisement
MATESO YANGU- SEHEMU YA KWANZA
 
Mtunzi: Deo Massawe 0653195298.
Mhariri: William Shechambo

Ilikua Alhamisi majira ya jioni, ambapo Joseph alikua na mwanawe aitwae Dennis ndani ya gari wakirejea nyumbani ambapo ilikua desturi ya Joseph kumpitia mtoto wake kila siku shuleni, mara baada ya kukamilisha mizunguko yake mjini.

Dennis alikua na umri wa miaka 4 ila alikua mjanja sana na alikua mwenye akili iliyotosha kumuuliza baba yake maswali mengi sana kuhusiana na maisha yao.

Moja maswali ambayo Denis alikua anamuuliza baba yake ni kuhusiana na yeye kutokumjua mama yake.

Kila mara alikuwa akimbana Baba yake kwa maswali, “Baba, hivi mama yupo wapi mbona haji nyumbani hata sikukuu kutusalimia?”

Swali hilo lilimchosha sana baba Dennis, maana lilikua linamkumbusha machungu kwa sababu mama yake Dennis alifariki kwa ugonjwa wa Ukimwi miezi 6 tu, baada ya kumzaa Dennis ila baba yake aliamua kumficha kwa kumdanganya mwanae kuwa yupo.

Kila ilipokutana na maswali ya Dennis alikuja na jibu, "Mama yupo safarini na atakuja tu siku yoyote." (Huku akishindwa kuzuia machozi yaliyoonekana wazi wazi yanadondoka)
Kiukweli Dennis alikua anashangaa sana na kujiuliza, "Mbona baba kila napokuuliza hili swali unajibu alafu unalia au nawe umemmis mama? sasa mwambie aje maana hata me nimemmis".

Baba Dennis ili kueouka maswali zaidi, alikuwa anaondoka sebuleni au popote na kuingia ama chumbani au jikoni kuandaa chakula huku akimwagiza Dennis afanye Homework yake ya shuleni na kuufanya mjadala wa MAMA uwe umefungwa.
*
Chakula kiliikua tayari na wakaanza kula, wakati wa kulala Dennis na baba yake hulala kila mtu chumba chake pamoja na umri wa Dennis kuwa mdogo, alilala chumba chake.

Siku moja kabla ya kwenda kulala, Dennis alimwambia baba yake, "Baba Jumapili twende huko mama aliko tukamsalimie sisi kama yeye amegoma kuja."

Baba alimjibu kwa kutikisa kichwa kutoka chini kwenda juu kama ishara ya kuafiki na hapo kila mmoja akaenda kulala.

Ila baba Dennis kiuhalisia, alikua mtu wa kuendekeza starehe sana kwa hiyo akiagana na mtoto muda w akulala, yeye hutoka na kwenda viwanja kula starehe lakini kamwe hakuwahi kusahau jukumu lake kama Baba hivyo huwahi kurudi asubuhi na mapema ili kumwandaa mtoto wake kwa shule.
*
Jumapili asubuhi na mapema Dennis na baba yake walikua na gari aina ya Toyota Corolla tayari kwenda kwa Mama huku mawazo ya baba Dennis akiwaza atamuonesha mama yupi hata kumdanganya tu mwanawe.

Baada ya kuwaza sana, akaona amdanganye kwa kumpeleka ufukweni hivyo akapanga safari ya kuelekea fukwe za Coco jijini Dar es Salaam, akihisi kuwa wakifika huko basi mwanaye atasahau habari ya mama.

Safari ilianzia Car wash kwanza, kuosha gari lakini kwa bahati mbaya mwosha gari akaloanisha siti ya mbele pembeni mwa dereva ambayo ndo siti aliyotakiwa kukaa Dennis.

Kiti hicho, ni kama kilikuwa kimeandikwa jina la Dennis kwa sababi kamwe hakuwahi kukaa pengine tofauti na hapo kwenye gari ya Baba yake, lakini kutokana na hilo ilimbidi akubali kukaa nyuma ili safari iendelee akamuone Mama yake.

Safari ya kwa Mama ilianza....Gari iliondoka kwa kasi kubwa eneo hilo huku akili za Dennis zikimwaza Mama, wakati zile za Baba zikipanga kuwahi fukwe za Coco kabla vibanda vya kuuzia mihogo havijafungwa.
*
Puuuuuuuuuuh! ndicho Dennis alichosikika akikisema Dennis kwa madaktari wa hospitali ya taifa Muhimbili (MNH), mara baada ya kuzinduka kutoka azimie kwa saa kadhaa kutokana na ajali mbaya sana waliyoipata akiwa na Baba yake.

Gari yao iligongana uso kwa uso na Lori la mizigo kwenye makubano ya Barabara ya Kilwa na Baba yake alikufa pale pale lakini Dennis alinusurika akiwa hana hata jeraha kubwa zaidi ya michubuko midogo midogo.
*
Mipango ya mazishi ilianza na kutokana na baba Dennis kuendekeza starehe, alikua kaitenga sana familia yake na kuwa karibu na wanawake wakiponda raha.

Ilikamilika kwa kufikia maamuzi ya kumzika na sehemu iliyoafikiwa na familia ilikuwa ni nyumbani kwao Morogoro.

Dennis naye akawa amebaki yatima ila yeye hakujua na aliamini kua kwenye mazishi ya baba yake basi Mama yake atakuja hapo.
 
Hivyo aliwaza kuwa licha ya kwamba amepoteza Baba, Mama yupo na angefurahi sana kumuona hatimaye.

Jumatano iliwadia. asubuhi na mapema... msafara wa gari ya maiti na baadhi ya ndugu wa Baba Dennis ulianza kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro kwenye mazishi.

Dennis alionekana mwenye huzuni sana lakini moyoni mwake haikuwa hivyo, kwani alikua na kiasi fulani cha furaha kama maandalizi ya furaha isiyokifani kumuona mama yake msibani.
*
Mweno wa saa 6, walikua kijijini Morogoro ambako walikuta watu wakiomboleza kwa majonza makubwa sana. Dennis mtoto pekee wa Baba Dennis alikua mbele ameshikilia msalaba wakati wa kuingiza maiti kwenye nyumba ya familia.

Baada ya kufika eneo hilo wakati vilio vikiwa vimetawala kila kona, Dennis yeye hapo ndo furaha ilizidi kwani aliamini muda si mrefu atatokea Mwanamke ambaye atatambulishwa kwake kama Mama Dennis.
****
ITAENDELEA.
Je, unadhani nini kitatatokea ? Dennis atafanyaje baada ya kuja kugundua Mama yake hayupo hai, atalelewa na nani kwa sababu tayari ni yatima? Ungana nasi kwa sehemu ya pili ya simulizi hii ya kusisimua
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: