Advertisement |
Siku chache tangu kuibuka kwa vuguvugu la viongozi wa CHADEMA mkoani Arusha kubwanga manyanga, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Arusha ,
umesema kauli iliyotolewa na Katibu wa CHADEMA kanda ya Kaskazini, Aman
Golugwa, ikidai viongozi wa UVCCM wamewanunua madiwani wao
waliojizulu ni za uongo.
Amesema madai hayo hayana ukweli hata kidogo na kwamba UVCCM inamtaka Golugwa kuthibitisha taarifa hizo zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwa ushahidi vinginevyo
watachukua hatua kali dhidi yake.
Katika mkutano wa waandishi wa habari na CHADEMA
uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha, Golugwa alikaririwa akisema mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya UVCCM mkoa wa Arusha, Joshua
alimwambia kuwa "Tutawashughulikia tumekusanya fedha kutoka kwa wafanya
biashara zaidi ya milioni 200."
Pia alisema kwa bahati mbaya mjumbe huyo hajui kutunza siri na kwamba amemuoa binamu yake Golugwa.
Akisoma tamko la UVCCM mkoa wa Arusha katibu wa UVCCM mkoa
wa Arusha Said Goha mbele ya kamati ya utekelezaji ya UVCCM mkoa na
waandishi wa habari alisisitiza CCM ni chama kikongwe hakijahusika na
hakitahusika kwa namna yeyote ile kuwarubuni wadiwani wa upinzani
kujiuzulu nafasi zao na kwamba wanafanya hivyo kwa utashi wao wenyewe.
Kwa mujibu wa Goha katika taarifa hizo wamesema taarifa za
kununuliwa kwa madiwani hao Golugwa alitibitishiwa na mjumbe mmoja wa
kamati ya utekelezaji ya UVCCM aliyemtaja kwa jina moja la "Mwarabu"
tunaomba wazithibitishe wa ushahidi.
Akiendelea kunukuu kauli hizo, Goha alisema CHADEMA imesema
mjumbe huyo ameoa binamu yake na katibu huyo wa CHADEMA kanda ya
Kaskazini ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA mkoa.
"Tunaomba amtaje kwa
jina mke huyo na uthibitisho wa cheti cha ndoa au kielelezo chochote," alisema.
Goha alisema katika maelezo yake katibu Golugwa alidai madiwani hao wamenunuliwa kwa mamilioni ya shilingi hivyo walimtaka ajitokeze ili ataje kiwango cha
fedha na uthibitisho wa madiwani waliopokea fedha hizo.
Kwa mujibu wa Goha, Golugwa alisema diwani wa Ngabobo
Solomon Laizer aliileza CHADEMA kuwa barua ya kujiuzulu hakuandika yeye
wala sahihi iliyoko kwenye barua hiyo siyo ya kwake.
"UVCCM tunamuomba
diwani huyo ajitokeze hadharani kuthibitisha au kukanusha kauli hiyo," alisema.
Aidha, UVCCM umeitaka CHADEMA kutambua kuwa CCM ni chama
kikongwe kimepitia kwenye misukosuko mingi na bado kipo imara hakiwezi
kutetereka na kwamba madiwani waliokuwa wa CHADEMA wakajiuzulu hata
wangeendelea kubaki CHADEMA hawaizuii serikali ya CCM kuendelea
kutekeleza ilani yake.
"Niwakumbushe tu CHADEMA kuwa mwenyekiti wao wa taifa
Freeman Mbowe hivi karibuni alisema kuwa katika uchaguzi mkuu wa 2015
walifungua milango na madirisha na kuacha kila aina ya mdudu
kuingia, sasa wanaotoka wasiituhumu CCM kwa kutafuta mchawi watambue
wachawi ni wao wenyewe," alijinasibu.
Aidha alitumia fursa hiyo kuitaka CHADEMA kuangalia walipojikwaa badala ya kuangalia walipoanguka.
Pamoja na hayo, aliitaka CHADEMA kujiuliza kama wanachama wa chama hicho kwa mikoa
mingine wanaohamia CCM kama wamenunuliwa pia kama anavyoodai ama lah.
"Au tuwaulize CHADEMA mawaziri
wakuu wastaafu Fredrick Sumaye na Edward Lowassa na mzee Kingunge na
wengine wengi CHADEMA imewanunua kwa shilingi ngapi?" alihoji.
Shechambo blog ilipomtafuta Golugwa kwa simu, jitihada ziligonga mwamba baada ya simu yake kutokuwa hewani kwa muda mrefu mpaka habari hii inakamilika kuandikwa.
0 comments: