Advertisement |
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet
Hasunga (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza
alipotembelea shamba la miti Sao Hill kukakua shughuli mbalimbali zinazofanywa
na shamba hilo mkoani Iringa hivi karibuni. Aliagiza uongozi wa shamba hilo
kuongeza juhudi za upandaji miti ili kukidhi mahitaji makubwa yaliyopo nchini
na hivyo kusisimua ukuaji wa uchumi wa viwanda.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe. Japhet Hasunga
(kulia) akikagua baadhi ya vifungashio vya asali alipotembelea shamba la miti
Sao Hill kwa ajili ya kukakua shughuli mbalimbali zinazofanywa na shamba hilo
mkoani Iringa hivi karibuni. Asali inayozalishwa na shamba hilo imefanyiwa
vipimo nchini Ujerumani na kugundulika kuwa ni bidhaa bora isiyo na viambata
vya kemikali ya aina yeyote. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza
na Afisa Ufugaji Nyuki wa shamba hilo, Said Abubakar.
Meneja wa shamba la miti Sao Hill, Salehe Beleko
(kushoto) akimueleza Mhe. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga
(kulia) kuhusu moto uliovamia hekta 77 za shamba hilo na hatua
zilizochukuliwa kuudhibiti alipotembelea
kukakua shughuli mbalimbali zinazofanywa na shamba hilo mkoani Iringa
hivi karibuni, alisema moto huo uliozuka hivi karibuni ulianzia kwenye mashamba
ya wananchi haukuwa na madhara makubwa.
Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill, Salehe Beleko
(kulia) akimuelezea Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe. Japhet Hasunga kuhusu utafiti unaofanywa na shamba hilo kwa kushirikiana na Kampuni ya Art
International kuhusu uvunaji wa utomvu kwa ajili ya kutengeneza madawa
mbalimbali, bazooka (chewing gums) na ‘gel’ kwa ajili ya kujiongezea kipato
alipotembelea shamba hilo kukagua shughuli mbalimbali hivi karibuni. Kushoto ni
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Mhe. Jamhuri David.
Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill, Salehe Beleko
(kulia) akimuelezea Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe. Japhet Hasunga (hayupo pichani)
kuhusu njia mpya ya kuzalisha mbegu za miti kwa njia ya vikonyo ili kuongeza
zaidi uzalishaji alipotembelea shamba hilo kukagua shughuli mbalimbali hivi
karibuni. Aliagiza uongozi wa shamba hilo kuongeza juhudi za upandaji miti ili
kukidhi mahitaji makubwa yaliyopo nchini na hivyo kusisimua ukuaji wa uchumi wa
viwanda.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet
Hasunga (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza (wa pili
kulia) alipotembelea Kituo cha Mambo ya Kale cha Ismila kukakua shughuli
mbalimbali zinazofanywa na kituo hicho mkoani Iringa hivi karibuni. Wa pili
kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mhe. Richard Kasesela.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili
kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza (kushoto) wakipata maelezo
kutoka kwa Mhifadhi wa Mambo ya Kale, Laurent Nampunju (kulia) kuhusu fuvu la
Chifu Mkwawa alipotembelea Makumbusho ya chifu huyo kukakua shughuli mbalimbali
zinazofanywa na kituo cha Mambo ya Kale cha Kalenga mkoani Iringa hivi
karibuni.
Jengo la Makumbusho ya Mkwawa ambalo lipo ndani ya Kituo cha Mambo ya Kale cha Kalenga Mkoani Iringa.
Picha ya Chifu Mkwawa ambayo inapatikana katika makumbusho hayo.
Muonekano wa fuvu la Chifu Mkwawa ambalo pia linapatikana katika makumbusho hayo. (Picha na Hamza Temba - WMU)
0 comments: