Advertisement |
Bodi
ya Usajili wa Wakandarasi Nchini (CRB), imewatahadharisha wananchi,
watu wenye miradi ya ujenzi pamoja na wakandarasi nchini kuwa makini na
watu wanaotumia jina la bodi hiyo kufanya utapeli.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msajili wa bodi hiyo, Rhoben Nkori (Pichani), imewataka wananchi na wakandarasi wawe wanatoa taarifa katika ofisi
za bodi za Makao Makuu Dar es Salaam na Kanda zake ili kuwakamata na
kuwafikisha mahakamani watu wa aina hiyo.
“CRB
ina ofisi za kanda ambazo zinafanya kazi nchi nzima, kanda hizo ni
Kanda ya mashariki – Dar es salaam, Kanda ya kaskazini Arusha, Kanda ya
kusini Mbeya, Kanda ya ziwa Mwanza na Kanda ya kati Dodoma, watumie ofisi hizi wasirubuniwe na matapeli,” alisema Nkori.
Aidha,
alisema watumishi wa CRB wamekuwa wakienda kwenye ukaguzi wakiwa na
vitambulisho vya bodi hiyo na vizibao vyenye nembo ya CRB
vinayowatambulisha kuwa wanatoka bodi hiyo.
Alisema
kuna watu ambao wamekuwa wakijiita wawakilishi wa Bodi hiyo na kufanya
shughuli za bodi hiyo kwa njia ya utapeli na kuchukua rushwa kwa
wakandarasi na wenye miradi.
Kwa
mujibu wa maelezo yaliyotolewa leo Julai 16 na CRB, watu hao wamekuwa wakijitambumbulisha kama wawakilishi wa bodi hiyo ambao huwa wanakwenda
kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi maeneo mbalimbali.
Alisema
watu hao hutembelea sehemu zenye miradi na kuwatisha watu wanaofanya
shughuli za ujenzi na kuwaomba rushwa ili wasiwashtaki wanapobaini
kasoro kwenye miradi yao.
Aidha,
alisema watu hao wamekuwa wakiwaandikia barua watu wenye miradi ya
ujenzi wajieleze kwanini wasichukuliwe hatua na bodi kwa kufanyakazi zao
bila kuzingatia masharti ya ujenzi kama vile kuweka vibao vya kuonyesha
mkandarasi anayejenga.
“Sisi
CRB hatuwatambui watu hao na tunawaomba wananchi na watu wenye miradi
ya ujenzi wawe makini na wakiwa na tatizo waende kwenye ofisi za kanda
zetu ambazo tumezitaja kama kuna watu anahisi wanataka kumtapeli
awasiliane na bodi ili tumkamate na kumfikisha mahakamani,” alisema
Blog hii ilifanikiwa kupata nakala ya barua yenye nembo ya CRB
iliyoandikwa na mmoja wa matapeli hao kwenda kwa mmoja wa wateja akidai
kutaka ufafanuzi wa baadhi ya mambo kwenye mradi wake wa ujenzi
unaoendelea.
Kwenye barua hiyo kwenda kwa mteja tapeli huyo aliandika hivi “ I need the following drawings, architectural drawing, structural drawing and Building permit and sign board.
“Hapo
anamaanisha kuwa mteja huyo amuonyeshe mchoro wa jengo, kibali cha
ujenzi na kibao ambacho kisheria kinapaswa kuwekwa sehemu ya ujenzi
kikionyesha jina la mteja, mkandarasi, mhandisi mshauri na
mkandarasi,” alisema.
0 comments: