Tuesday, July 18, 2017

Makundi 21 ya WhatsApp yachunguzwa

ad300
Advertisement
Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa nchini Kenya, imetangaza kuwa inachunguza makundi 21 ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp , yanayosambaza ujumbe wa chuki na uchochezi wakati huu ambao ni wiki chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, mwezi ujao.
 Mwenyekiti wa tume hiyo, Francis Ole Kaparo, amesema tayari wameanza mchakato wa kuwahoji wamiliki wa makundi hayo ya Whatsapp kutoka kaunti 21 nchini humo.

Kaparo amesema tume yake itawafungulia mashtaka wale wote wanaochochea au kutuma ujumbe wa chuki kwa lengo la kuzua machafuko kabla na baada ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Agosti 8.
 Serikali ya Nairobi kwa uoande wake imeweka msisitizo wa agizo hilo la tume kuwa, haitakubali watumiaji wa mitandao kuvuruga amani kwenye uchaguzi wa mwaka huu kwa kueneza habari za uvumi na uchochezi.


Wakati huo huo, Francis Wangusi, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kenya, amevionya vyombo vya habari nchini Kenya kuepuka kutangaza matokeo ya uchaguzi kabla ya tume ya kusimamia uchaguzi na mipaka kufanya hivyo.

Kwa upande wa vyombo vya usalama, Inspekta Jenerali wa Polisi, Joseph Boinet, amesema polisi watatumia nguvu kiasi kuwakabili wachochezi wa ghasia iwapo fujo zitatokea. 

Onyo lake linakumbusha matukio ya mwaka 2007/08 wakati polisi walipotuhumiwa kuhusika na  mauaji ya kiholela walipokuwa wakikabiliana na ghasia.

Aidha, wakati hayo yakiripotiwa, wasiwasi umeendelea kutanda katika Kaunti ya Lamu kutokana na kuongezeka mashambulio ya wanamgambo wa kundi la Al-Shabab katika siku za hivi karibuni.

Sambamba na hayo, kampeni za uchaguzi zimeendelea kupambana moto huku vyama vikuu vya Jubilee na Muungano wa NASA vikiendelea na kuumana kona zote za nchi kuomba kura za wananchi.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: