Advertisement |
Kufuatia mapigano yaliyotokea mjini Kinshasa, mji
mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, vyama viwili vya siasa
washirika vinavyounda serikali ya nchi hiyo, vimetaka kutangazwa hali ya
hatari nchini.
Imesemekana kuwa baada
ya mapigano makali Ijumaa iliyopita katika soko la mjini Kinshasa,
chama cha (PRPD) na chama tawala nchini humo vimetoa taarifa ya pamoja
ya kutaka kutangazwa kwa hali ya hatari nchini kwa kutegemea kipengele
cha 144 cha katiba.
Katika ripoti hiyo, vyama hivyo vimesisitiza kuwa,
DRC inahitaji mshikamano kwa ajili ya
kupambana na kile kilichotajwa kuwa ni ugaidi.
Wakati huo huo, wapinzani wa serikali
wamepinga na kukosoa suala hilo na kusema kuwa, kutangazwa hali ya
hatari kuna maana ya kuzuiwa uhuru sambamba na kutoa mwanya wa
kuahirishwa tarehe ya uchaguzi mkuu nchini.
Hii ni katika hali ambayo
Tume Huru ya Uchaguzi nchini humo imetangaza hivi karibuni juu ya kuwepo
uwezekano wa kuahirishwa kwa tarehe ya uchaguzi mkuu nchini
humo.
Christophe Lutundula, mmoja wa wanasiasa wa upinzani na mjumbe wa
kundi la vyama saba vya kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(G7), sambamba na kutangaza upinzani wake juu ya pendekezo hilo la
serikali kwa ajili ya kuahirishwa uchaguzi mkuu, amesema hatua hiyo inachukuliwa kwa lengo la kutaka kumbakisha madarakani
zaidi Rais Joseph Kabila.
Amesema kuwa, kuahirishwa uchaguzi, ni
kinyume na katiba na hata makubaliano ya Desemba 31, mwaka 2016, yaliyofikiwa kati ya serikali na vyama vya upinzani.
Kwa mujibu wa
makubaliano hayo, Rais Joseph Kabila anatakiwa kuondoka madarakani
ifikapo Desemba mwaka huu.
0 comments: