Monday, July 17, 2017

United, Arsenal na Chelsea usipimee

ad300
Advertisement
Wababe wa soka nchini England, Manchester United, Arsenal na Chelsea zimetuma salamu kwa wapinzani wao katika msimu mpya wa Ligi Kuu.

Timu hizo juzi usiku zilivuna ushindi mnono katika mechi za kirafiki za kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu England 2017/2018.

United ilibuka na ushindi mnono wa mabao 5-2 katika mchezo dhidi ya LA Galaxy ya Marekani.Mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Drake Arena, Marekani ulikuwa wa aina yake ambapo straika mpya, Romelu Lukaku, alicheza.

Kinda wa United, Marcus Rashford, alionyesha kiwango bora baada ya kufunga mabao mawili na kutengeneza nafasi mbili za mabao yaliyofungwa na Enrikh Mkhitariyan na Marouane Fellaine.

Mfaransa Anthony Martial, alihitimisha karamu ya mabao kwa kufunga la tano na Giovani dos Santos, alifunga mabao mawili ya Galaxy.

Pia mabingwa wa Kombe la FA, Arsenal ilivuna mabao 3-1 kwenye Uwanja wa ANZ, Australia dhidi ya Western Sydney.

Arsenal ilipata mabao kupitia kwa Olivier Giroud, Mohammed Elneny na Aaron Ramsey kabla ya nyota wa Sydney, Steven Lustica, kufunga bao la kufutia machozi.

Chelsea kwa upande wake iliendelea kutakata baada ya kufanya kufuru kwa kushinda mabao 8-2 dhidi ya Fulham United inayocheza Ligi Daraja la Kwanza England kwenye Uwanja wa mazoezi Cobham.

Mabao ya mabingwa wa Ligi Kuu ya England yalifungwa na wachezaji Willian da Silva (matatu), Michy Batshuayi (mawili), Loic Remy (mawili) na Cesar Azpilicueta.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: