Advertisement |
Taifa Stars ilikuwa mwenyeji wa mchezo huo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, ukiwa wa kwanza kuwania kufuzu Fainali za Kombe la CHAN zitakazochezwa mwakani.
Akizungumza kwa simu kutoka Mwanza, kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga (Pichani), alisema wachezaji walikamia kupata matokeo bora hatua iliyowagharimu.
Mayaga alisema timu hiyo ilicheza chini ya kiwango na ameona upungufu katika safu ya ushambuliaji na ulinzi, lakini atayafanyia kazi kabla ya timu hizo kurudiana Julai 23, mwaka huu.
“Timu ipo vizuri lakini katika mchezo huu wachezaji waliingia uwanjani kutafuta ushindi na kujisahau kupambana hadi wakaruhusu goli kuingia.
Nimeona mapungufu mengi kwenye kikosi changu hasa nafasi ya ushambuliaji, nitahakikisha nafanyia kazi kujiandaa na mchezo wa marudiano ili tuweze kupata ushindi,” alisema Mayanga.
Pamoja na hayo, Mayanga alisema hataki kurudia makosa hivyo atahakikisha anakinoa vizuri kikosi chake ili kushinda mchezo wa marudiano mjini Kigali.
Wakati huo huo, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, alisema timu hiyo itaendelea kuweka kambi Mwanza hadi Julai 19 ambapo itakwenda Rwanda kwa ajili ya mchezo wa marudiano.
Lucas alisema Taifa Stars itaanza mazoezi leo asubuhi na jioni kwa ajili ya kujiweka fiti.
“Timu itasafiri Julai 19 lakini itabaki Mwanza kujiandaa na mchezo wa marudiano na Rwanda utakaochezwa Julai 23 mwaka huu,” alisema Lucas.
Taifa Stars itakuwa wageni katika mchezo huo na timu hiyo italazimika kushinda mjini Kigali ili kusonga mbele katika kuwania tiketi ya kucheza michuano ya CHAN mwakani nchini Kenya, ambako itamenyana na mshindi kati ya Sudan Kusini na Uganda zilizotoka suluhu.
0 comments: