Monday, July 17, 2017

'Ndoa' ya TBC, Star Times kuchunguzwa

ad300
Advertisement
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ameunda kamati ya kuchunguza ubia wa Kampuni ya StarTimes na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), kufuatia hoja mbalimbali zilizojitokeza.

Kamati hiyo iliyotangazwa mwishoni mwa wiki na Waziri Mwakyembe, itaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk. Hassan Abbasi.Itakuwa na wajumbe 10, watakaochunguza utendaji wa
Kampuni ya Ubia ya StarTimes, ambapo watano ni wa upande wa Tanzania na wengine kutoka Star Media ya China.

Wajumbe wanaounda kamati hiyo kwa upande wa Tanzania ni Dk. Hassan Abbasi na Kyando Evod (Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo), Frederick Ntobi na Mhandisi James Kisaka (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania-TCRA) na Mbwilo Kitujime (Shirika la Utangazaji la Taifa-TBC).

Kutoka Star Media China, majina yao yatawasilishwa kutoka nchini humo ili kukamilisha idadi kamili ya wajumbe 10 wa kamati hiyo.Kamati hiyo imepewa hadidu za rejea takribani nane na inatakiwa kufanya kazi kwa muda wa siku saba ili kukamilisha kazi hiyo.


Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: