Monday, July 17, 2017

Harusi ya Mbunge 'yapakwa' mayai

ad300
Advertisement
BRASILIA, Brazil
Mbunge wa Panara, Maria Barros (25) ambaye ni mtoto wa Waziri wa Afya wa Brazil, ameonja joto ya jiwe baada ya waandamanaji kuharibu harusi yake kwa kumrushia mayai viza akiwa kanisani.

Hatua hiyo ilifuatia kitendo cha mwanasiasa huyo nchini Brazil kuwakashifu waandamanaji wa mrengo wa kushoto kwa kuwadhulumu wageni wakati wa harusi hiyo kufuatia familia yake kumuunga mkono Rais Michel Temer.

Mamia ya waandamanaji walikusanyika nje ya kanisa ambamo sherehe za harusi ya mbunge huyo zilikuwa zikifanyika na kuanza kurusha mayai yaliyoharibika jambo lililovuruga sherehe hiyo.

Kutokana na vurugu hizo, mwanasiasa huyo alilamizimika kuondoka kanisani hapo akitumia gari lisilopenya risasi.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na wanasiasa wa nchi hiyo, akiwemo baba yake Ricardo Barros na mama yake Cida Barghetti ambaye ni naibu gavana wa Parana.

Takriban wabunge 30 wa nchi hiyo walialikwa kusafiri kutoka mji mkuu Brasilia kuhudhuria harusi hiyo kwenye mji mkuu wa jimbo la Parana, Curitiba.

Picha za tukio hilo zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha walinzi wakifungua myamvuli kuwakinga wageni na bwana harusi dhidi ya mayai walipokuwa wakiondoka kanisani hapo.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: