Sunday, July 16, 2017

BRELA sasa kidijitali

ad300
Advertisement
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), unatarajia kuzindua mfumo wa usajili wa kampuni na biashara kwa njia ya mtandao.

Baada ya mchakato wa muda mrefu, mfumo huo utazinduliwa mwezi ujao lakini kila Mtanzania atapaswa kuwa na kitambulisho kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili kuhudumiwa kwa urahisi.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Frank Kanyusi (Pichani), amesema wageni kutoka nje ya nchi mara baada ya kuzinduliwa kwa mfumo huo watatakiwa kutumia namba za pasipoti zao za kusafiria.

Awali, huduma ya mtandao ilikuwa ni kwa ajili ya majina ya biashara lakini sasa imepanuliwa na kuruhusu usajili wa majina ya kampuni.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: