Advertisement |
Chama kikuu cha upinzani hapa nchini CHADEMA, kimetangaza kumuunga mkono Rais Uhuru
Kenyatta wa Kenya katika uchaguzi mkuu ujao uliopangwa kufanyika Agosti 8
mwezi ujao.
Wajuzi wa mambo wanaamini kuwa, chama cha upinzani cha Chadema kinamuunga mkono Rais Kenyatta, kutokana na uhusiano wa karibu ulipo kati ya Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga.
Msimamo huo umetangazwa na Edward
Lowassa, Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye
pia aligombea kiti cha urais kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi
uliopita wakati alipofanyiwa mahojiano maalumu na kusisitiza kuwa, Uhuru
Kenyatta ni chaguo bora la demokrasia nchini Kenya.
Lowassa ambaye alikuwa Kenya kushiriki
mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya Joseph Ole
Nkaissery amemtaja Uhuru Kenyatta kama mtu mzurim anayeunga utangamano
katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na ambaye anawawaheshimu viongozi wa
upinzani.
Wajuzi wa mambo wanaamini kuwa, chama cha upinzani cha Chadema kinamuunga mkono Rais Kenyatta, kutokana na uhusiano wa karibu ulipo kati ya Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga.
Freeman Mbowe, Mwenyekiti Taifa wa
CHADEMA alinukuliwa mwezi Mei mwaka huu akimtaja Raila Odinga kuwa ni
msaliti kutokana na kumuunga mkono Rais Magufuli.
Mbowe alinukukuliwa akisema kuwa, katika
uchaguzi wa mwaka 2013 nchini Kenya, tulimuunga mkono Raila Odinga,
lakini tulishangazwa mno katika uchaguzi wa mwaka 2015 nchini Tanzania
wakati Odinga alipotangaza kumuunga mkono mgombea uraia kwa tiketi ya
CCM John Pombe Magufuli.
0 comments: