Friday, May 26, 2017

WB yamwaga fedha elimu bure

ad300
Advertisement

Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia (WB), imekubali kupitisha kiasi cha dola za kimarekani milioni 80 (sh. Bilioni 176) kwa ajili ya kuiunga mkono serikali ya Tanzania kwenye mpango wake wa elimu bila malipo kuanzia ngazi ya elimu ya awali mpaka kidato cha nne.

Msaada huo umetolewa kupitia mpango wa WB unaojulikana kama EPforR, ambao unasimamiwa na Chama cha Kimataifa cha Maendeleo (IDA), ambao awali ulijulikana kwa jina la Matokeo Makubwa Sasa ukilenga sekta ya elimu na nyingine kadhaa.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana kutoka jijini Washington nchini Marekani, ilisema WB imeridhishwa na mpango huo mpya wa serikali ya Tanzania unaotekelezwa kwa kipindi cha miaka 11 kuanzia 2016, ambao unachukuliwa na Tanzania kama njia mojawapo ya kuufikia uchumi wa viwanda  kabla ya mwaka 2025.

Ilisema tangu kuanza kwa mpango huo wa elimu bila malipo, imeshuhudia mzigo mkubwa wa wanafunzi kwenye shule mbalimbali za msingi na sekondari, changamoto ambayo WB imeamua kuitatua kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania kupitia sera zake mbalimbali.

Taarifa hiyo pia ilisema kiasi hicho cha fedha kinakusudiwa kusaidia Tanzania kuongeza jitihada kwenye usimamizi wa mpango huo hasa kwa kutoa nafasi zaidi kwa wanafanzi wakike kujiunga na elimu ya msingi na sekondari ili kuhakikisha usawawa jinsi unazingatiwa sambamba na utoaji wa elimu bora.

Akizungumza baada ya uamuzi huo wa bodi, Mwakilishi mkazi wa WB nchini Tanzania, Bella Bird, alisema fedha hizo zitakuwa na msaada mkubwa kwa serikali ya Tanzania ambayo imeamua kuondoa vizuizi vya upatikanaji wa elimu kwa wananchi wake kuanzia ngazi ya elimu ya msingi mpaka sekondari.

“Tunaipongeza serikali ya Tanzania kwa kuondoa vizuizi vya upatikanaji wa elimu hasa kwa jamii masikini, huku pia ikizingatia utoaji wa elimu bora iliyokuwa ikihitajiwa na wengi," alisema Bella anayesimamia shughuli za WB katika nchi za Somalia, Malawi, Burundi na Tanzania.

Mradi huo ulioanzishwa rasmi na WB, Julai 2014, ukianza na kiasi cha dola za kimarekani milioni 122, huku ukiwa na malengo ya kuboresha elimu kwa ngazi ya elimu ya msingi na sekondari, unatekelezwa pia na serikali za Sweden na Uingereza kwa kutumia vyanzo vyao vya ndani.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: