Advertisement |
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadick,
amepiga marufuku tabia inayofanywa na Wafugaji ya kuhamisha mifugo kutoka
kijiji kimoja kwenda kingine na kudai kuwa kufanya hivyo kunaweza kusababisha
maambukizi ya magonjwa kwa mifugo.
Sadick
alitoa kauli hiyo jana, alipofanya ziara katika Jimbo la Moshi vijijini, na
kuongea na Wananchi wa kata ya Mabogini ambapo alisema wafugaji wamekuwa
wakihamisha mifugo kutoka kijiji kimoja kwenda kingine na kusambabisa kusambaa
kwa magonjwa ya mifugo.
Alisema
pia kuhamishwa kwa mifugo hiyo kumekuwa sababu kubwa ya migogoro ya Wakulima na
Wafugaji hivyo ni vyema kila mmoja akafuata sheria na taratibu zilizowekwa kwa
kuheshimiana bila kujali kazi ya mwenzake.
“Chanzo
cha migogoro ya ardhi ni kuhamishwa kwa mifugo kutoka kijiji kimoja kwenda
kingine na kulishwa katika mashamba ya wakulima huku Serikali ya kijiji
ikiwafumbia macho.
“Hivyo
kuanzia leo napiga marufuku biashara ya kuhamisha mifugo kutoka sehemu moja
kwenda nyingine bila kuwa na kibali maalum cha unapota na kule unapoelekea,”
alisema Sadick.
Aidha
mkuu huyo wa mkoa aliwataka viongozi wa Serikali ya vijiji kuweka mipango ya
matumizi ya ardhi kwa kugawa sehemu ya wakulima na wafugaji ambapo itasaidia
kupunguza tatizo la migogoro ya wakulima na Wafugaji.
Kwa
upande wake Diwani wa kata ya Mabogini, Emmanuel Mzava, alisema kuwa
wanakabiliwa na tatizola chakula katika shule za msingi na sekondari zilizopo
katika kata hiyobaada ya baadhi ya Wazazi kukataa kuchangia chakula ili
Wanafunzi wale chakula cha mchana bure.
Mzava
alisema tatizo lingine linaloikabili kata hiyo ni migogoro ya ardhi baina ya
wakulima na Wafugaji, ambapo Wafugaji kutoka katika vijiji vya jirani wamekuwa
wakileta mifugo yao na kuingiza katika mashamba ya wakulima na kusababisha
migogoro ya mara kwa mara.
Kwa
upande wa wananchi, waliiomba Serikali kuwagawanyia jimbo hilo baada ya
kumlalamikia Mbunge aliyepo sasa Anthony Komu
(Chadema), kutowapigania na kuwasemea matatizo yao Bungeni watu wa tambarare na
badala yake amekuwa akiwapigania watu wa milimani.
0 comments: