Friday, September 9, 2016

Mtibwa, Simba kuvaana VPL leo

ad300
Advertisement
Timu ya soka ya Simba saa chache kuanzia sasa itavaana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Mchezo wa leo unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka kutokana na historia iliyopo kwa timu zote mbili.Simba itaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda mchezo wa mwisho dhidi ya Ruvu Shooting ambapo walishinda mabao 2-0.

Akizungumza Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, alisema kuwa wataingia katika mchezo huo wakiwa na tahadhari kubwa kwani Mtibwa sio timu ya kubeza.
 

Alisema kuwa wamefanya mazoezi ya kutosha na wachezaji wao wapo fiti na wana ari kubwa ya mchezo huo.
 

Manara alisema kuwa lengo la Simba msimu huu ni kuhakikisha wanafanya vizuri kila mechi ili kujitengenezea mazingira mazuri.
Alisema kuwa mashabiki wanatakiwa kujitokeza kwa wingi ili kutoa ushirikiano kwa timu yao iweze kufanya vizuri.
 

“Mtibwa sio timu ya kubeza kwani pia inawania taji, hivyo tutaingia uwanjani tukiwa na tahadhari kubwa ili kuhakikisha tunashinda, mashabiki waje kwa wingi kutoa hamasa kwa wachezaji,” alisema.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: