Friday, September 9, 2016

Wanne wajeruhiwa ajali iliyohusisha msafara wa M/Rais

ad300
Advertisement
Msafara wa makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, umepata ajali eneo la Nanguruwe, nje kidogo ya mji wa Mtwara. 
Ajali hiyo ilitokea baada ya gari lililokuwa limewabeba wasaidizi wa Makamu wa Rais kuacha njia na kupinduka.

Kwa mujibu wa Katibu wa Makamu wa Rais,  msafara ulikuwa unaelekea wilayani Tandahimba ukitokea Ikulu ndogo ya Rais iliyoko Mtwara mjini.

Katika ajali hiyo watu wanne akiwemo dereva wa gari husika wamejeruhiwa na wamekimbizwa hospitali ya rufaa ya Ligula kwa matibabu zaidi.

Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa rais kuacha njia na kupinduka, gari lililokuwa limebeba waandishi wa habari wa channel ten, star tv na clouds tv liliacha njia na nusura kupinduka.

Mashuhuda wa tukio wanasema barabara ya kutoka Mtwara kwenda Tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha.

Wamesema hali hiyo inasababisha magari yaliyo kwenye mwendokasi kuacha njia mara kwa mara na mengine kupinduka.

Shechambo Blog inawatakia majeruhi wote nafuu ya haraka,  Amen.
Gari iliyokuwa kwenye msafara wa Makamu wa Rais mara baada ya kuacha njia na kupinduka
Majeruhi wa ajali hiyo wakipewa huduma ya kwanza
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: