Sunday, September 11, 2016

Serikali kuibana TFF

ad300
Advertisement
Waziri Nape Nnauye akiwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, imeagiza Mkaguzi Mkuu wa Serikali kufanya ukaguzi wa rasilimali watu na rasilimali fedha ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania, TFF.

Serikali imefikia uamuzi huo kutokana na kuibuka kwa mijala mbalimbali kuwa kuna ufujaji wa fedha ndani ya TFF.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, alimwagiza Mkaguzi Mkuu wa Serikali kufanya mchakato huo ili wadau wa michezo waweze kupata majibu ya mijadala waliyonayo.
Alisema kuwa kumekuwa na mijadala mbalimbali inayoendelea juu ya ufujaji wa fedha ndani ya TFF.


“Namwagiza Mkaguzi Mkuu wa Serikali popote alipo aje kufanya ukaguzi wa rasilimali watu na rasilimali fedha ndani ya TFF ili kuondoa mijadala inayoendelea,” alisema.


Nape alisema kuwa anaipongeza TFF kutokana na kuratibu michuano mbalimbali.Waziri huo alisema kuwa pia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), kudhibiti vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu wa TFF ambao utafanyika Oktoba mwakani.
 

Alisema kuwa TAKUKURU inatakiwa kujikita katika vyanzo vya rushwa kuanzia mikoani ili TFF ifanye uchaguzi huru na wa haki na kupata viongozi waadilifu.
 

“Tunaiomba pia TAKUKURU, ianze kusimamia vyanzo vya rushwa kuanzia katika mikoa kuelekea uchaguzi ili kupata viongozi waadilifu.
 

Serikali itasimamia uchaguzi huo kuhakikisha wanapatikana viongozi ambao wataendeleza michezo nchini,” alisema.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: