Advertisement |
BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA), limesema
litaanza kutumia mfumo wa wastani wa pointi (GPA) katika upangaji wa ufaulu kwa
watahiniwa wa kidato cha nne na sita.
Hatua ya kutumika viwango hivyo ilifikiwa na Bodi ya
NECTA katika mkutano wa 98 na tayari serikali imeridhia kutokana na kuonekana
kuwa na viwango.
Kuanza kutumika kwa mfumo huo, kutasaidia kukuza
kiwango cha elimu na kuondoa malalamiko kutoka kwa wadau wa elimu wakiwemo
wanafunzi.
Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonda,
alisema juzi mjini Dar es Salaam, kuwa mfumo huo ni rahisi kueleweka na
utasaidia kupunguza malalamiko kuhusiana na viwango vya ufaulu.
Alisema katika upangaji wa matokeo ya mtahiniwa
mfumo wa GPA utatoa tafsiri itakayoonyesha kuwa mwenye GPA kubwa ndiye
aliyepata matokeo mazuri na mwenye GPA ndogo ndiye aliyekuwa na ufaulu wa
chini.
"Utaratibu wa kuandika GPA huandikwa katika nafasi moja ya desimali na nafasi ya pili ya desimali hukadiriwa katika makumi ya karibu," alisema huku akitolea mfano wa GPA ya 3.15 kuwa sawa na 3.2 na GPA ya 3.14 kuwa sawa na 3.1.
Alisisitiza katika mfumo wa makundi alama ya juu ya
ufaulu itaanzia A 75-76 ambayo ni bora sana, B+ 60-74, Vizuri sana, B 50-59
Vizuri, C 40-49 Wastani, D 30-39 Inaridhisha, na F 0-19 ambayo ni feli.
Aliongeza kuwa mtahiniwa aliyepata daraja la kwanza
la pointi saba kwenye mfumo wa jumla ya pointi, atapewa daraja la ufaulu bora
sana (Distinction) kwa wastani wa pointi 5.0 pindi ukokotoaji wa madaraja ya
ufaulu utafanyika kwa kutumia mfumo wa wastani.
Dk. Msonde alisema baada ya mabadiliko hayo
wameshirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha ufanisi zaidi katika
mfumo huo.
Pia, wameanza kusambaza elimu kwa wadau kuhusiana na
mfumo huo.
0 comments: