Sunday, September 7, 2014

Benki kuu yatoa sarafu mpya ya 500/=

ad300
Advertisement
BENKI kuu ya Tanzania (BOT), imetangaza kuingiza sarafu mpya ya Shilingi mia tano, kwenye mzunguko wa fedha kuanzia mwezi oktoba mwaka huu.

Hatua hiyo imetokana na noti iliyopo ya fedha hiyo, kutumika katika mzunguko kwa muda mrefu bila ya kurejeshwa kwenye mabenki kwa wakati muafaka, kwa kubadilishwa pindi zinapofikia ukomo wake hali inayochangia kuchakaa zaidi kwa noti hiyo.

Sarafu hiyo mpya iliyotengenezwa kwa madini ya chuma na Nickel, itakuwa na umbo la duara lenye michirizi pembezoni, upenyo wa milimita 27.5, uzito wa gramu 9.5 na sura ya Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Sheikh Abeid Aman Karume.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana, Mkurugenzi wa Masuala ya Kibenki wa BOT, Emmanuel Boaz, alisema utengenezwaji wa sarafu hiyo umezingatia thamani ya fedha hiyo na madini yaliyotumika kutengenezea.

Alisema uzingatiaji huo umelenga kuhakikisha sarafu hiyo kuibaki kuwa na thamani zaidi kuliko madini yaliyotumika kutengenezea ili kuzuia baadhi ya watu kutumia sarafu hiyo kinyume na matumizi yaliyokusudiwa.

"Kama madini yaliyotumika kutengenezea yakiwa na thamani zaidi ya sarafu yenyewe ni raisi kwa watu kuitumia kama malighafi nyingine." alisema

Aidha, Boaz alisisitiza kuwa, fedha hiyo itaendelea kutumika sambamba na noti zilizopo za sasa mpaka noti hizo zitakapokwisha katika mzunguko wa fedha.

Benki kuu ya Tanzania ndiyo chombo chenye jukumu la kutoa fedha halali kutumika nchini, ikiwa na lengo la kurahisisha upatikanaji wa chenji, mahitaji ya bidhaa na huduma kwa  wananchi ili kupata katika mafungu ya fedha yatakayo kidhi mahitaji yao.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: