Sunday, August 31, 2014

Afa kwa kuanguka akiezeka.

ad300
Advertisement
FUNDI Mwashi aliyefahamika kwa jina la Ramadhan Pilipili (52), mkazi wa Karakata jijini Dar es Salaam, amekufa baada ya kuanguka kutoka kwenye paa la nyumba aliyokua akiiezeka.

Tukio hilo lilitokea juzi saa mbili kamili asubuhi, maeneo ya Viwege, Chanika nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam wakati fundi huyo akiwa kwenye harakati za kupaua nyumba hiyo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Mary Nzuki, alisema upelelezi wa awali ulionyesha kuwa fundi huyo alikufa papo hapo mara tu baada ya kuanguka kutoka kwenye paa hilo.

Alisema hakuna taarifa zingine zilizopatikana kuhusiana na tukio hilo ikiwemo sababu ya fundi huyo kuanguka, hadi hapo upelelezi utakapokamilika.

Kamanda Mary alisema mwili wa marehemu ulihifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) huku upelelezi ukiendelea.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: