Sunday, April 6, 2014

Wanne wapoteza maisha ajalini Dar..

ad300
Advertisement
WATU wanne wamekufa na wengine watano kujeruhiwa baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kugongwa na kupinduka eneo la Uwanja wa Taifa, Temeke mkoani Dar es Salaam.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Englibert Kiondo alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 2.00 asubuhi ikiyahusisha magari mawili moja likiwa ni Volvo na. T 198 AJL lenye tela na. T 198 ACF, likiendeshwa na Hemed Ndegele na jingine ni Suzuki Carry na. T 177 CLY lililokuwa likiendeshwa na Ally Mfaume (29).

Kamanda Kiondo aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Shoya Jumanne (30), Samuel Rashid(27), Koroma na Vincent walifahamika kwa jina moja kila mmoja ambapo wote walikadiriwa kuwa kati ya miaka 25 mpaka 30.

Alisema Volvo lilipokuwa likitoka Kiwanda cha Serengeti kwenda Bandarini, lilihama njia na kugonga gari aina Suzuki Carry iliyokuwa imebeba abiria tisa na kusababisha vifo vya watu hao wanne papo hapo.

Kwa mujibu wa Kiondo maiti zimehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke, na watu wengine watano walionusurika pia walifikishwa Hospitalini hapo kwa matibabu.

Alisema upelelezi juu ya tukio hilo unaendelea na Jeshi hilo limemshikilia Dereva wa Volvo.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: