Advertisement |
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi (W) Temeke | Sophia Kanega akipanda mti kwenye Hospitali ya Vijbweni. |
Sophia Kanega akiwa na moja ya zawadi za Vitenge walovyovitoa juzi. |
Katibu wa Jumuia hiyo Suleiman Ndende alisema kwa kawaida siku hiyo huadhimishwa Aprili 6 ya kila mwaka lakini wao kama Wilaya waliiadhimisha kabla ili waweze kujumuika na wenzao wa mkoa jana.
Akiongoza shughuli hiyo Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Temeke Sophia Kanega pamoja na wajumbe wengine walipanda miti ya Kivuli katika Hospitali ya Mbagala na kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo sabuni za kufulia kwa wagonjwa waliokuwepo hospitalini hapo.
Pia waliitembelea Shule ya Msingi Mianzini iliyopo katika Manispaa ya Temeke ili kuona matatizo yanayoikabili shule hiyo na jinsi ya kuyatatua kwa kuyafikisha ngazi za juu za Serikali kwa manufaa ya watoto ambao ni taifa la kesho.
Sambamba na hilo pia waliizawadia Hospitali ya Vijibweni mashine mbili za kupimia magonjwa ya Moyo na Sukari kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo Hospitalini hapo.
Sophia alisema wao kama Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Temeke wameamua kuwa mfano kwa Wilaya zingine katika utendaji kazi kwa lengo moja la kuisaidia jamii hususan mashuleni na hospitalini kila mara inapopata wasaa wa kufanya hivyo.
Akizungumza baada ya kumaliza shughuli hizo za kijamii, Katibu wa Siasa na uenezi Wilaya ya Temeke Rutami Masunu alisema katika ziara hiyo ameona kero kadhaa ambazo wao kama Viongozi wanatakiwa wazitatue kwa ajili ya Wananchi.
Alisema kuna uhaba wa Madarasa kwenye Shule ya Mianzini, pamoja na eneo katika Hospitali ya Mbagala ambayo inalihitaji kwa ajili ya upanuzi wa hospitali hiyo inayohudumia Wananchi wengi kwa sasa hivyo Serikali sikivu iliyo chini ya Uongozi wa CCM itaendelea kuzitatua.
0 comments: