Sunday, April 6, 2014

Benki ya ACB yawabeba Wajasiriamali

ad300
Advertisement

Innocent Ishengoma (Katikati) na Mwenzake wakimuelezea mmoja wapo wa Mjasiriamali aliyeshiriki Mkutano huo faida za kutumia huduma za bank yao.
BENKI ya Akiba Commercial (ACB) imewataka Wajasiriamali wanawake kutosita kutumia huduma za benki hiyo kwakua ndiyo pekee nchini inayokidhi haja za Mjasiriamali anayehitaji mafanikio endelevu katika biashara yake kwa karne hii.

Pia wametakiwa kutambua kuwa benki hiyo ya Kitanzania ilianzishwa kwa ajili ya Wajasiriamali wa chini na wa kati ili kuwasaidia kifedha kupata mafanikio kwa kufahamika kitaifa na kimataifa.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Afisa Masoko wa benki hiyo Innocent Ishengoma kwenye Mkutano na maonesho ya Wajasiriamali Wanawake yaliyofanyika katika hotel ya Mbezi garden na kudhaminiwa na benki hiyo.

Ishengoma alisema ACB imekuwa mstari wa mbele kuwajali Wajasiriamali nchini tokea kuanzishwa na wengi wamefanikiwa kutokana na kutumia huduma zao rafiki kwa Mjasiriamali za kuweka akiba na utoaji wa mikopo.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na Wajasiriamali wanawake zaidi ya mia moja wakiongozwa na taasisi ya Tanzania Business Empowerements for Women (TBEW), chini ya Mwenyekiti wao Haika Lawere, wengi walifurahishwa na kuomba fursa hiyo mara kwa mara.

Mmoja wa washiriki Binti Shangwe, alisema baadhi ya manufaa waliyoyapata pamoja na elimu kutoka kwa ACB, kampuni ya  GS1 ambayo inahusika na utoaji wa Barcodes kwenye bidhaa na watu kutoka Shirika la viwango nchini (TBS), wameongeza  wigo wa biashara kwa kufahamiana na watu.

Akizungumza na Washiriki hao, Meneja mikopo wa ACB Salome Mwakigomba alisema Mjasiriamali anatakiwa asiwe na uwoga wa kukopa katika taasisi za fedha hususan Akiba Commercial Bank lakini awe na nidhamu kwa kutokujiingiza kwenye mkopo zaidi ya Benki moja.

Salome alisema mkopo hauepukiki kwa mtu anayehitaji maendeleo katika Maisha hasa Mjasiriamali lakini anatakiwa aijali biashara yake kwakua biashara na mmiliki havitenganishiki.

Meneja mikopo huyo pia alitoa wito kwa Wajasiriamali hao wanawake kujenga mahusiano mazuri kwa kila anayehusika katika biashara yake zikiwemo taasisi za kifedha hususan katika suala la uaminifu kwakua ndio chachu ya mafanikio kibiashara.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: