Monday, July 24, 2017

Serengeti yatembelewa na mabilionea wa dunia

ad300
Advertisement

Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe, amewapokea Mabilionea 26 katika Mbuga ya Serengeti.

Mabilionea hao walifuatana na wenzi wao (26) katika ziara yao ya siku 3 nchini Tanzania.

Wageni hao ambao wanatoka katika club ya  mabilionea  ya YPO (Young Presidents Organisation)  wanatoka mabara yote duniani.

Ziara hii ni ushahidi kuwa Tanzanina sasa hivi inaongoza kwa vivutio vya utalii barani Afrika na dunia kwa ujumla.

Katika ziara hiyo ya nchi nane (8) ambazo ni: Uingereza, Rwanda, Tanzania, Maldeves, Nepal, Bhutan, Rajastan na nchi moja nyingine, wageni hao wamemwaga sifa kemkem kwa vivutio vya Tanzania.

Katika hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia Wageni wake, Profesa Maghembe aliwakaribisha nchini Tanzania na kuwaambia maajabu ya Dunia yamebebwa na hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

"Hakuna eneo lolote katika uso wa Dunia lenye mkusanyiko wa wanyama wanaokula majani (herbivorous) na wale wanaokula nyama (carnivorous) kama ilivyo katika mbuga hiyo ya Serengeti," alisema.

Aidha, Profesa Maghembe aliwaeleza wageni wake kuwa uhifadhi ni gharama kubwa inayobebwa na Tanzania kwa niaba ya Dunia.

Aliwaomba wageni hao wawe Mabalozi wa kuitangaza Tanzania kama eneo pekee la amani lenye vivutio vyenye ubora wa pekee duniani.

Waziri huyo alisema hatua hiyo italeta watalii wengi nakuiongezea Tanzania mapato.

Aidha, aliwaomba warudi tena kuwekeza nchini ili washiriki kwenye uchumi unaokuwa kwa wastsni wa 7% kwa kipindi cha miaka 15 sasa.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: