Tuesday, April 15, 2014

Serikali yaboresha mifumo Sekta ya Sheria

ad300
Advertisement
SERIKALI imeongeza idadi ya watendaji kwenye Sekta ya Sheria nchini ili kutatua tatizo la mlundikano wa kesi kwenye Mahakama nchini.

Imeelezwa kuwa Januari 2007, Serikali ilikuwa na jumla ya Waendesha mashitaka 95 nchi nzima lakini leo imewaajiri zaidi ya rasilimali watu 400 wenye majukumu ya kuendesha Mashitaka.13

Hayo yalisemwa jana na Mwendesha  Mashitaka Mkuu wa Serikali (DPP), Eliezer Feleshi wakati wa Mahojiano maalum katika kipindi cha Kituo kimoja cha Televisheni nchini.

Mwendesha Mashitaka huyo alisema hatua hiyo imekuja baada ya kufanyika mabadiliko makubwa ya mfumo wa utendaji katika Sekta hiyo kupitia ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kipindi cha miaka saba iliyopita kuanzia 2007.

Alisema kuwa nia hasa ni kuongeza tija kwenye mfumo wa uendeshaji wa kesi za jinai ambapo unatakiwa uwe madhubuti, na  umekuwa ukitumiwa na Serikali tokea 2007 kuanzia hatua ya upelelezi mpaka kesi inapofika Mahakamani.

Feleshi alisema awali watendaji wachache walikuwa wakitumia muda mwingi wa kutimiza wajibu wao, kufanya shughuli zaidi ya moja ikiwa ni njia mojawapo ya kumsaidia Mkurugenzi wa Mashitaka wa Serikali lakini sasa wamepatiwa mamlaka ya kufanya shughuli husika bila kufungwa na majukumu mengine kwa namna yoyote.

Alisema Serikali ilipitisha Sheria ya uendeshaji wa Mahakama mapema 2008 ili kurekebisha mapungufu yaliyokuwapo kwenye Sekta hiyo muhimu nchini, ambapo mafunzo yatakuwa yakitolewa kwa watendaji husika wa upelelezi wa makosa ya jinai na kufanya tathmini kila mwisho wa mafunzo.

Aidha alisema mwanzoni mwa mwaka 2007, Serikali ilikuwa ikiendesha kesi kwenye mikoa 13 kutokana na uhaba wa rasilimali lakini sasa kutokana na maboresho yaliyofanywa, jumla ya vituo kwenye mikoa 23 vinasikiliza kesi bila tatizo kutokana na kuwepo kwa waendesha mashitaka kwenye kila makao makuu ya Mikoa.

Sambamba na hilo alisema Juni 2007, kwa wastani kulikuwa na wafungwa na mahabusu 42,000 lakini leo wastani ni 34,935 kwasababu idara za serikali na wadau wameboresha utoaji wa hakijinai kuzingatia katiba ya nchi.

Alisema matokeo mengine ya uboreshwaji wa mfumo wa Sheria nchini yameonekana katika Mahakama ya Kisutu kwakua wastani wa kesi kwa mwaka 2007-2008 ulikuwa ni kesi 2000 kwa mwaka lakini sasa hata kesi 500 kwa mwaka hazifiki.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: