Friday, April 13, 2018

Simba 11 walishwa sumu

ad300
Advertisement
KAMPALA, UGANDA

SERIKALI ya Uganda imeshtushwa na tukio la Simba jike watatu na watoto wao wanane kukutwa wamekufa kwenye hifadhi ya taifa ya Queen Elizabeth, kutokana na kile kinachodaiwa kulishwa chakula chenye sumu.

Hifadhi hiyo ni moja kati ya hifadhi maarufu nchini humo ambayo inapatikana eneo la kusini magharibi mwa mji mkuu wa Ugnada, Kampala.

Taarifa kutoka nchini humo zilisema jana kuwa Mamlaka ya hifadhi ya Uganda, ilisema kuwa ucuhunguzi wa awali wa kitaalamu umebaini simba hao walililishwa nyama yenye sumu.

Idadi ya simba kwenye hifadhi ya Queen Elizabeth inakadiriwa kufikia 100 baada ya kifo cha simba hao watatu na watoto wao huku jumla ya simba kwenye hifadhi zote nchini humo ikikadiriwa kuwa 400.

Hifadhi za Uganda zinatajwa kuwa moja kati ya vyanzo vikubwa vya mapato yanayotokana na utalii, lakini mara kadhaa kumekuwa na mvutano kati ya wahifadhi na wananchi kutokana na suala la muingiliano wa mipaka.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: