Friday, April 13, 2018

Rais atangaza siku tatu za maombolezo

ad300
Advertisement
SERIKALI ya Algeria imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku tatu, kufuatia ajali ya ndege ya jeshi la Algeria iliyoua watu zaidi ya 250, baada ya kuangua juzi Aprili 11, karibu na uwanja wa ndege wa Buteflika, ikiwa ni dakika chache baada ya kuruka.

Akizungumza kwenye televisheni ya taifa ya nchi hiyo jana jioni, Rais Abdelaziz Bouteflika, alisema kwa siku hizo tatu bendera ya nchi hiyo itapepea nusu mlingoti huku akiagiza sala ya leo kwenye misikiti yote kuwa maalumu kuwaombea waliopoteza maisha.

Taarifa kuhusu ajali hiyo ziliripotiwa na shirika la habari la Ennahar la nchini Algeria, ambapo zilisema ndege hiyo ya jeshi aina ya Ilyushin II-76, ilianguka katika barabara inayounganisha uwanja wa ndege wa Buteflika na Blida.

Msemaji wa kikosi maalumu kinachohusika na kutoa huduma katika matukio ya dharura nchini humo, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema miongoni mwa waliofariki kwenye ajali hiyo ni raia wakiwemo watumishi wa ndege hiyo, askari na wajumbe 26 wa kundi la Polisario.

Ajali hiyo inatajwa kuwa mbaya zaidi kutokea nchini humo katika kipindi cha miaka 10, huku ikihusisha idadi kubwa ya watu wakiwemo askari watiifu wa serikali ya Algeria.

Bado haijaelezwa chanzo hasa cha ajali hiyo, huku mamlaka mbalimbali zikiendelea na jitihada za kupeleleza chanzo na sababu halisi ya kutokea kwa ajali hiyo mjini Bilda.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: