Friday, April 13, 2018

Fedha, Teknolojia na muingiliano wake

ad300
Advertisement
FEDHA ni kitu kilichokubaliwa na watu wa eneo fulani kitumike kama njia ya kubadilishia huduma, bidhaa na rasilimali.

Kwenye kila eneo, yaani nchi au ukanda kuna fedha ambayo jamii yake imekubali kuitumia kama sehemu ya mbadilishano.

Zamani, kabla ya maendeleo ya teknolojia historia inasema hakukuwa na fedha, watu walikuwa wanatumia bidhaa kubadilishana;

Kwa mfano, mtu alikuwa anatoa mfuko wa mchele kwa mtu mwenye mfuko wa maharagwe na hapo yeye anakuwa amepata bidhaa aliyokuwa akiihitaji kwa wakati husika.

Mfumo huu ulikuwa mzuri kwa wakati ule, lakini kadri muda ulivyosogea na watu kuongezeka, kukaibuka tatizo la watu kuhitaji bidhaa ambayo kwa wakati huo mtu anayo, lakini anakosa mtu mwingine mwenye bidhaa anayoihitaji kwa wakati husika.

Hapo likaibuka wazo la kuwepo kwa kitu mbadala ambapo kabla ya fedha, kulikuwa na wazo la fedha-bidhaa ambapo chumvi, chai, tumbaku, mbegu za mazao, zilitumika kama 'fedha' za kupata bidhaa nyingine.

Kipindi hiki chote, bado teknolojia haikutambulika kama inaweza kubadili takriban kila tatizo la binadamu likiwemo hilo la kuwa na kitu au njia rasmi na ya kuaminika ya kubadilishana bidhaa, huduma na rasilimali miongoni mwa jamii.

Muda haukwenda sana kabla ya watu wenye akili kugundua kuwa fedha yaani sarafu na noti ndio suluhisho la kudumu la binadamu kwenye suala zima la kutafuta njia ya kubadilishana bidhaa, huduma na rasilimali, ambapo kati ya mwaka 5,000 KK na 700 KK jamii ya watu walioitwa Walidia wakawa jamii ya kwamba kuwa na fedha yao.

Tangu hapo, sarafu za kila umbo na thamani ziligunduliwa na jamii mbalimbali, huku madini ya chuma ndio yalikuwa malighafi rasmi ya kutengenezea sarafu hizo kwa sababu inadaiwa yalikuwa madini rahisi kufua na kuundia kitu, kisha baadaye kubadili tena matumizi yake.

Fedha za karatasi inadaiwa zilianza kuonekana barani Asia katika nchi ya China, kuanzia kipindi cha miaka 960 BK na kuendelea, ambako teknolojia yao iliwaruhusu kuzitengeneza katika maumbo makubwa tofauti na ilivyo sasa.

Maisha ya fedha yaliendelea huku yakiongezewa nguvu na maendeleo ya teknolojia duniani, ambapo mataifa mbalimbali yaliweza kutengeneza fedha zao kwa msaada mkubwa wa teknolojia ambapo, zimekuwa na alama zinazoweza kusomwa na mashine za kielekroniki ili kuzuia utamaduni mbaya wa wajanja kughushi fedha hizo.

Ni kutokana na maendeleo hayo ya teknolojia, watu duniani waliamua kutambulisha aina nyingine ya fedha inayojulikana kama Cryptocurrency, ambayo kimsingi ndio haswa darasa langu kwako kwa siku ya leo.

Kitafsiri, Cryptocurrency ni aina ya fedha ya ya kidigitali ambayo imeundwa kuwa salama na mara nyingi, katika mazingira yasiyojulikana.

Ni sarafu inayohusishwa na intaneti inayotumia mifumo ya msimbo na mchakato wa kubadili habari ya halali katika msimbo ulio mgumu kuvunjika, katika kufuatilia manunuzi na uhamisho wa thamani.

Teknolojia inayotumika katika kutengeneza na kusambaza Cryptocurrency inaitwa kwa jina la ‘Blockchain’ ambayo kwa tafsiri rahisi ni sanaa ya kuandika na kusoma msimbo, iliyozaliwa kutokana ya haja ya mawasiliano salama katika kipindi cha Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Utaalamu huo umebadilika katika ulimwengu wa sasa wa kidigitali ukiwa na vipengele vya nadharia ya hisabati na sayansi ya kompyuta kuwa njia ya kupata mawasiliano, habari na fedha mitandaoni.

Cryptocurrency ya kwanza ilikuwa Bitcoin, ambayo iliundwa mwaka 2009 na ndiyo ambayo bado inajulikana zaidi kuliko zingine.

Inaelezwa kuwa kumekuwa na usambaaji wa Cryptocurrency mbalimbali katika kipindi cha miaka 10 iliyopita na mpaka sasa kuna zaidi ya 1,000 zilizopo kwenye mtandao ambapo thamani yake inazidi kukua kila siku.

Kimsingi, ‘Blockchain’ ni mkusanyiko wa vitalu vya taarifa za miamala ambazo haziwezi kuharibika, kutokana na kuhifadhiwa kwenye maelfu ya kompyuta duniani kote.

Mbali ya kuhifadhi taarifa za miamala ya fedha, mkusanyiko huu wa taarifa huweza kutengenezwa ili kuhifadhi taarifa za kitu kingine chochote chenye thamani kama vile dhahabu na madini mengine yenye thamani duniani.

Mtandao wa Blockchain unafanya kazi katika hali ya makubaliano baina ya watumiaji na ukilinganisha taarifa moja kwa moja na vitalu vingine kila baada ya dakika kumi kwa uwezeshwaji wa teknolojia ya TEHAMA.

Ina mfumo wa ukaguzi wa kujitegemea wa mihamala ya kidigitali. Mtandao huu unalinganisha na kupatanisha kila mihamala inayofanyika. Blockchain haiwezi kudhibitiwa na chombo au taasisi yoyote.

Inadhaniwa pia  teknolojia hii inaweza kuongeza ufanisi na kupunguza gharama kuwezesha uandikaji wa mikataba rahisi ambayo inaweza kutekelezeka katika mazingira maalumu.

Kwa kuwezesha malipo baina ya pande mbili, wadau wanasema kwamba teknolojia ya Blockchain inafungua mlango wa kuingiliana kwa moja kwa moja kati ya pande mbalimbali zinazoshiriki katika uchumi.

Wafuasi wa teknolojia hii wanaona na wanasema kwamba Blockchain inaruhusu mihimili ya utawala kuwa wazi zaidi na kuthibitishwa wakati wa kusimamia mali, vitegauchumi na taarifa zilizo katika mfumo wa kielektroniki.

Ni Salama?

Hofu ya kwanza ni juu ya mazingira ya usiri yanayohusisha teknolojia ya blockchain hasa katika Bitcoins.

Kuna maswali machache ya msingi ambayo hayawezi kujibiwa kirahisi; kwa mfano: Kutojulikana kwa mwasisi wa bitcoins. Hali hii inaongeza hatari katika udhibiti katika suala la kuruhusu au kukuza teknolojia.

Kwa mujibu wa uchunguzi juu ya usiri unaozunguka teknolojia hii, kuna uwezekano wa kuwepo na hali ya juu ya kutozingatia mahitaji.

Ukweli wa kuwa kwamba teknolojia hii haiwezi kudhibitiwa na chombo kimoja husababisha tishio kubwa na hatari kwa kufuata udhibiti.

Kutoka na mtazamo wa kuingizwa kifedha, teknolojia haiwezi kuathiri kwa njia nzuri idadi kubwa ya watu ambao hawapatikani kifedha.

Nini kifanyike kuhusu Cryptocurrency?

Kuchukua hatua za tahadhari na kutaarifu umma juu ya hatari zilizopo kwa kushiriki katika masuala yanayohusiana na cryptocurreny;

Taasisi zinazohusika na fedha nchini kama vile BoT, zinapaswa kuendelea kutafiti na kujifunza teknolojia hii kwa kina kwa lengo la kutafuta suluhisho la kudumu ambalo limezingatia mahitaji ya udhibiti wa masuala ya fedha ya nchi.

Mbali na hayo, ni muhimu kuwajengea uwezo wafanyakazi wanaohusika na usimamizi wa masuala yanayohusu huduma za kifedha zinazotumia teknolojia (ikiwamo cryptocurrency) ili kuweza kusimamia udhibiti ipasavyo.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: