Friday, March 9, 2018

Zimamoto JNIA kutoa mafunzo endelevu

ad300
Advertisement
Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kitaendelea kutoa mafunzo ya uzimaji moto na uokoaji kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na ofisi zote zinazofanya shughuli zake kwenye kiwanja hicho.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa kituo hicho, Kamishna Msaidizi Juma Yange wakati wa kufunga mafunzo ya zimamoto na uokoaji yaliyofanyika kwa washiriki kupata nadharia na baadaye vitendo yaliyofanyika kiwanja hicho.

Afande Yange amesema kwa kuwa wafanyakazi wengi hawajui namna ya kujiokoa wakati wa majanga ya moto, hivyo wanafanya mafunzo hayo kuwa endelevu kwa kuyafanya kuwa endelevu, endapo moto utatokea waweze kujiokoa na kuokoa mali.

“Mafunzo haya yana madhumuni ya kuwawez moto kwenye sehemu yake ya kazi, kufahamu vyanzo na vitu vinavyosababisha moto na vifaa vya huduma vya kwanza vya kuzimia moto vilivyopo eneo lake la kazi, hivyo litakuwa endelevu,” amesema.

Kwa upande wake, Bi. Julieth Fonga wa Kampuni  ya General Aviation Services inayofanya kazi zake katika jengo la Kwanza la abiria (TBI) la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ameomba mafunzo hayo kutolewa mara kwa mara ili kuwaweka tayari kwa janga hilo la moto.

Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo, Sajini Maria Gulam amesema wananchi wawe makini na moto, ambao unatokana na muunganiko wa kemikali unaofanywa na vitu vitatu kwa uwiano maalum, ambavyo ni joto, hewa safi na kiwashio.

Sajini Gulam amesema wananchi watambue kuwa moto upo katika madaraja manne ambayo ni ‘A' yenye viwashio vya asili kama majani, kuni, mkaa, karatasi; daraja ‘B' ina viwashio vya asili ya kimiminika kama mafuta taa, petrol, diseli, mafuta ya kula; huku daraja ‘C' ni asili ya gesi na ‘D' inatokana na michemko ya madini na hutokea zaidi kwenyte viwanda vya kutengeneza mabati, mitambo ya vipuri.

  • Hata hivyo, Sajini Gulam amesema mafunzo haya ya zimamoto na uokoaji yanatolewa kwa taasisi za umma na binafsi kwa gharama nafuu, ili waweze kujua namna ya kujiokoa na kupiga simu namba 114 ya kuomba msaada wa gari la zimamoto.



Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: