Thursday, March 8, 2018

Ujumbe wa Aysharose Mattembe (MB) kwenye siku ya wanawake duniani

ad300
Advertisement

"Wakati umefika kwa wanawake kushirikiana kuleta mabadiliko ya haraka kwenye sekta ya viwanda nchini.

Serikali ya Mhe. Dk. John Pombe Magufuli iko mstari wa mbele na utayari wa kuwawezesha wanawake kushika na uchumi wa viwanda kuanzia vidogo vidogo hadi vikubwa.

Kama Mwakilishi wa Wanawake wa Mkoa wa Singida, nilianza maadhimisho haya kwa kukutana na kuzungumza na wanawake wa Kiomboi,  kuhusiana na kujiunga kwenye vikundi ili kupata fursa ya mikopo katika kuwawezesha kuanzisha biashara, ujasiriamali na hatimaye kuwa wamiliki wa viwanda.

Pia tulifanya usafi maeneo mbalimbali na baadaye kupata changamoto za wafanyabiashara wadogo wadogo wanawake, ambazo nitakwenda kuzipatia ufumbuzi ndani ya Bunge letu tukufu.

Kama Kauli Mbiu ya Siku ya Mwanamke Duniani kwa mwaka huu inavyosema: Kuelekea Uchumi wa Viwanda, Tuimarishe Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji Wanawake Vijijini. 

Hakika hili linawezekana kwa pamoja tukiungana tutafanikisha."

Aysharose Mattembe.
Mbunge Viti Maalumu-Singida








Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: