Advertisement |
Naibu waziri huyo pia ameagiza vyombo vya usalama kufanya uchunguzi kwenye mradi huo ambao umechelewa kukamilika licha ya asilimia kubwa ya fedha kuwa zimeshalipwa kwa mkandarasi, lakini pia unakosa thamani halisi ya fedha zilizotumika katika ujenzi wake.
Aweso alitoa maagizo hayo wakati alipokuwa ziarani katika Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro mara baada ya kupata taarifa ya kusuasua kwa mradi huo na wananchi wa Gombe kukosa huduma ya maji kwa muda mrefu.
‘‘Katika taarifa nimeambiwa kuwa mradi unatoa maji, lakini nimekuja kuona na si kweli wakati wizara imetoa fedha. Kama Naibu Waziri wa Maji sitakubali kusikia fedha za miradi ya maji zinaliwa kila ninapoenda.
"Ninaagiza Mhandisi Mshauri akamatwe na uchunguzi ufanyike na endapo itabainika amehujumu achukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa wahandisi wote nchini," amesema Aweso.
Amesema wizara itaandaa orodha ya majina ya wakandarasi wote waliohujumu miradi ya maji na kuikabidhi kwa Bodi ya Usajili ya Wakandarasi (CRB), ili wafutiwe kabisa usajili na kutopewa kazi yoyote tena nchini endapo watathibitika kufanya hivyo.
Naibu waziri Aweso akiwa Ulanga amezindua ofisi ya maji ya Kata ya Lupiro, mradi wa maji wa visima 27 katika Kijiji cha Chikuti, ambacho ni moja ya vijiji vinavyonufaika na mradi huo na kukagua skimu ya umwagilaji ya Mnepa, iliyopo Kata ya Lupiro.
HABARI PICHA
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akishuka mara baada ya kukagua tenki la mradi wa maji wa Gombe, wilayani Ulanga, mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga wakiwa kwenye moja ya kichoteo cha maji cha mradi wa maji wa Gombe ambacho hakitoi maji.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa amebeba ndoo ya maji akiipeleka kwenye nyumba iliyopo katika Kijiji cha mara baada ya kuzindua mradi huo wa visima 27.
0 comments: