Friday, November 17, 2017

Watoto wa kitanzania watunukiwa Finland

ad300
Advertisement





Michoro ya watoto kutoka Tanzania yapewa tuzo nchini Finland

Michoro mitatu iliyochorwa  na watoto kutoka Tanzania hivi karibuni imetunukiwa tuzo ya heshima ya vyeti vya stashahada ya maonesho na Taasisi ya Sanaa za watoto na vijana ya Hyvinkää ya nchini Finland.

Watoto hao ni Bryton Manyewa (10), Neev  Mistry (9) wa shule ya Academic International Primary na Mandela Mtaya (5) wa shule ya Chekechea ya Upendo Montessori, manispaa ya Ilala.

Tuzo hizo zilitolewa kufiatia ushiriki wao katika shindano la michoro lililoitwa 'Pamoja' ambalo lilitayarishwa na taasisi hiyo ya nchini Finland.

Zaidi ya michoro 6, 800 kutoka katika nchi 66 duniani, zilishiriki shindano hilo ambapo majaji walikuwa ni wachoraji magwiji wa sanaa wa nchi hiyo.

Majaji hao walichagua michoro 670 kushiriki katika maonesho yaliyoanza Oktoba mwaka huu na kutarajiwa kufikia tamati Januari 18, 2018 nchini Finland.

Taasisi ya Hyvinkää inajihusisha na elimu ya Sanaa kwa watoto na vijana, ukuzaji wa muingiliano wa utamaduni wa nchi mbalimbali ambapo kwa miaka ya nyuma, kupitia ufadhili wa ubalozi wa Finland hapa nchini, baadhi ya watoto kutoka Tanzania walihudhuria mafunzo ya Sanaa yanayotolewa na taasisi hiyo.

Maonesho hayo yanaweza pia kutazamwa kupitia tovuti ya Taasisi hiyo ya www.artcentre.fi


Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: