Tuesday, September 5, 2017

Utabiri wa msimu wa vuli 2017

ad300
Advertisement
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa msimu wa mvua za vuli unaoanza Oktoba hadi Desemba mwaka huu. 
Kwa mujibu wa taarifa ya utabiri iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi mvua za Vuli zinatarajiwa kuanza mwezi huu wa Septemba. 
Mvua hizo ni katika maeneo mengi ya Ziwa Viktoria na mwezi Oktoba, maeneo ya ukanda wa Pwani na baadaye mwezi Novemba katika maeneo ya nyanda za juu Kaskazini Mashariki. 
Alisema ongezeko la mvua linatarajiwa katika miezi ya Novemba na Disemba, 2017 na hali kadhalika kutakuwa na vipindi virefu vya ukavu kujitokeza zaidi katika mwezi wa Oktoba, 2017. 
Hata hivyo alisema mvua zinatarajiwa kuwa za wastani katika maeneo mengi ya mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu, Shinyanga, Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Kilimanjaro, Arusha na Manyara, kaskazini mwa mkoa wa Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba. 
Dk. Kijazi alibainisha kuwa mvua za chini ya wastani na vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa kujitokeza hususan katika maeneo ya mikoa ya Kagera, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Pwani, Tanga, kaskazini mwa mkoa wa Morogoro pamoja na maeneo ya visiwa vya Unguja na Pemba. 
Pamoja na matarajio hayo ya mvua za wastani katika maeneo mengi ya nchi, uwezekano wa matukio ya vipindi vya mvua kubwa unatarajiwa hususan katika mwezi wa Disemba, 2017.

Mtawanyiko hafifu wa mvua na vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo katika kipindi cha msimu wa mvua wa Oktoba hadi Disemba, 2017 hususan katika maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Kilimanjaro, Arusha na Manyara, kaskazini mwa mkoa wa Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja and Pemba,” alisema. 
Pamoja na hayo, Dk. Kijazi aliwashauri wakulima katika maeneo hayo kuandaa mashamba yao mapema na kupanda mazao yanayokomaa katika muda mfupi, huku akizitaka mamlaka husika, kama vile wadau wa Afya, menejimenti za maafa, Mamlaka za miji na wadau wengine kuchukua hatua stahiki katika kupunguza athari mbaya zinazoweza kutokea katika msimu wa mvua za Vuli 2017. 
Aidha alisema kwa ujumala maeneo mengi yaliyopo kaskazini mwa nchi yanatarajiwa kupata mvua za wastani na uwezekano wa vipindi vifupi vya mvua kubwa hususan katika mwezi wa Desemba 2017. 
Msimu wa mvua wa Oktoba hadi Desemba (vuli) ni mahsusi kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka (Ukanda wa Ziwa Viktoria, nyanda za juu kaskazini mashariki, Pwani ya kaskazini na maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Kigoma). 
TMA inatarajia kutoa utabiri wa mvua katika maeneo  mengine ya nchi yaliyosalia baadaye Oktoba mwaka huu.  
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: