Tuesday, September 5, 2017

Simulizi ya kusisimua ya Mateso Yangu (EP 3)

ad300
Advertisement
MATESO YANGU- SEHEMU YA TATU
Mtunzi: Deo Massawe
Mhariri: William Shechambo

Asubuhi na mapema Bi Martha alitoka nyumbani kumfuta Dennis hospitali ili kujua maendeleo yake huku akijiuliza ni kwa jinsi gani mjukuu wake atakavyoendelea na maisha yake. 

Licha ya kuwa na mawazo mengi... Bibi alijipa imani kuwa mwanawe Joseph alikua tayari ameweka mazingira mazuri mwanae wa pekee jijini Dar es Salaam hivyo basi haitakua tatizo kumsomesha. 

Yeye ndo Mama na Baba wa Dennis kwa sasa... Mimi na wewe hatuwezi kulipinga hili. 

***

Jijini Dar es Salaam,  ndugu waliotumwa kufuatilia mali za Joseph ambao ni Haule na Joely walikurupuka asubuhi na mapema kama walivyozoea maisha ya kijijini ambapo huamka saa kumi alfajiri kwa ajili ya shughuli zao za kilimo ila wakashangaa mwenyeji wao hajaamka bado na hapo wakamwamsha kwa kumuita jina lake. 

 "Filbet kumekucha bwana mkubwa ni muda wa kuamka tukaanze kazi sasa hivi maana tunataka tuwahi nyumbani tukaangalie mifugo yetu" alisema Haule. 

Filbet aliwaambia walale kwa kuwa muda bado wa kuamka kwani yeye hakuwa na shida ya usafiri maana alikua na gari yake binafsi.

Hata hivyo Haule na Joely hawakulala bali waliamka na kutoka nje kuenda kupanga mipango yao maana walijua muda sio mrefu watapata pesa.
***
Bi Martha alimkuta mjukuu wake Denis akiwa katika hali nzuri, ni mkononi tu alikua na uvimbe ulotokana na kudondekewa jiwe kule kaburini ila mkono haukumzuia kuondoka naye,  hivyo walirejea nyumbani huku Dennis akiwa na majonzi sana ya kujigundua kuwa yeye ni yatima.

Walipofika nyumban basi Dennis alipewa chai na mkate iliyotoka kwa waombolezaji akanywa japo kwa shida nae bi Martha akawa anaongoza shughuli za kuomboleza pamoja na uzee wake bado alikua mkakamavu asieogopa kazi na watu wa mtaani walimwita bibi kijana na wakati mwingine aligombana na watu walomwita bibi.

***

Filbet aliendelea kulala huku akiwaza maisha aliyoishi na mambo waliyofanya na marehemu Joseph. 

Lakini ukweli ulikua marehemu Joseph enzi za uhai wake alikua anafanya biashara ya madawa ya kulevya akishirikiana na Filbet ambaye ndiye aliyetoka na akina Haule na Joely kijijini kuja kuhakikisha wanaokoa mali za marehemu.

Lakin pia siku chache kabla ya kifo cha Joseph kulikua na ugomvi kati ya marehemu na Filbet kutokana na kwamba marehemu Joseph alimfanyia dhuluma Filbet na Filbet hakufurahia hicho kitu na hapo ndipo alimtuma fundi gari kuenda kulegeza usukani wa gari ya marehemu Joseph ili akiendesha baada ya muda ipoteze mwelekeo na hapo ndo kitu kilichofanyika na kumfanya Joseph kupoteza maisha. 

Hivyo Filbet akaamini kuwa Joseph akifa atachukua mali zote kama kulipiza kisasi.... Kwa maana hiyo, akawa anawaza ni kwa jinsi gani ataweza kumiliki nyumba zote za marehemu Joseph maana aliamini hakuna mtu mwingne anaejua mali za marehemu.
***
Joely na Haule waliendela na maongezi yao, 
“Hivi ndugu yangu Joely kama ni pesa tumekuja kuokoa huku Dar es salaam ili tukamnufaishe huyu mtoto wa Joseph ambaye aliua ndugu zake wote wa damu na akauza maeneo yao yote na kutokomea huku mjini na sisi situlipize kisasi kwa kumiliki hii mali itakayopatikana?” Joely aliingiwa na huruma. 

"Kweli alifanyia watu unyama wa hali ya juu na mbaya zaidi alimuua hadi baba yake ila sasa mtoto wake sijui yule anaitwa Denis hana hatia na yatupasa tumwangalie kama mtoto wetu. " 

Haule akamweleze kwa umakini zaidi jinsi wakipata pesa watakavyoachana na maisha ya tabu za kijjiini na watakua watu maarufu mfano akamuonesha gari aina ya Land cruiser Toyota akamwambia nasisi tutanunua lakwetu kwani marehemu Joseph alinafanya makosa sana huku duniani hivyo mtoto wake anastahili ateseke.

Hapo Joely akaanza kutaman kuagana shida za kijijini hapo wakakubaliana kwa pamoja kua endapo wakipewa chochote basi watokomee nacho.
***
Filbert aliamka na kuingia bafuni na baada ya kuvaa alikaa sebuleni akachukua simu yake ya mkonononi na kuanza kufanya mazungumzo na makamanda wake wakubwa ambao ni Robert na Gerald hao ndio vijana alowaamini kwenye mauaji ya aina yoyote ndo vijana wake walioshinda kwenye mashindano ya kuua mtu kikatili ambapo walimuua mama mjamzito kwa kumtoboa tumbo na kuangalia jinsi mtoto anavyokaa tumboni na pia walikua maarufu kwa kuchukua madawa ya kulevya kutoka Pakistan hadi Afrika kusini.

Hapo Filbet akapewa taarifa kua tayari nyumba nne zishamilikiwa na vimada wa marehemu Joseph tena akajua wana hati halali kabisa isipokua ghorofa moja aliyoijenga maeneo ya Posta ndo ilikua na hati ya marehemu Joseph hapo hata Filbert akachanganyikiwa kusikia hivyo na akajisemea moyoni hiyo nyumba iliyobaki ni halali yangu ila hawa wanafamilia wa marehemu lazima wafe na sitaki wafie hapa mjini watawezaku niletea balaa. 

Filbert akachukua tena simu yake ya mkononi na kuwapigia tena vijana wake wa kazi.

"Oyo wakuu wangu kuna kazi jiandaeni mnasafiri kidogo kuna roho zaidi ya nne zinawahitaji ndani ya masaa matatu muwe hapa kwangu" Filbert alipanga kuwaua watu wanne yaan Joely, Haule, bi Martha na Dennis. 

Hapo baada yakukata simu aliwaita Haule na Joely ambapo kwa mda huo walikua nje wakisubiria kupewa pesa ili watokomee nazo hivyo waliingia ndani wakakaa na kupata kifungua kinywa.

***
Dennis alikunywa chai huku akiwaza kwa jinsi gani anavyoona watoto yatima wakiteseka mtaani na akafikiria jinsi akiwa na baba yake kwenye gari wanavoliliwa na watoto yatima wakitaka japo msaada wa chakula, yote hayo yalimuuma sana kugundua nae pia ni yatima.

Bibi yake alikuja na kukaa nae kumfariji kwa kumuondoa hofu kwani bibi alimpa uhakika wa kuisha maisha mazuri na hapo Dennis akafarijika. 
****
"Sasa ndugu zangu nimefanya mawasiliano na kugundua nyumba za huyu ndugu yenu marehemu Joseph alifanya makosa na aliandikisha hati za wanawake wake waliokua wanakula nae starehe kwa hiyo hapa sidhani kama kutakua na njia ya kuokoa chochote ila kuna pesa mimi nitawapa muhakikishe zinamfikia mtoto wa marehemu na mtajua jinsi ya kumhifadhia kwa hiyo ngoja tumpigie simu mwenyekiti wa kijiji chenu mumpe uhakika wa mambo yalivyo” Filbet aliongea kwa huruma sana kama malaika kwa kumuangalia huwezi kujua ni mtu mwenye roho mbaya zaidi ya mnyama. 

"Hallo ndugu mwenyekiti mimi hapa ni yule niliyejitolea kuja na vijana wa bi Martha kuja kufuatilia ile mali ya marehemu Joseph ila kwa bahati mbaya mali yote imetekwa na hakuna namna ya kuiokoa maana marehemu hakuisajili kwa jina lake lakin mimi nimejitolea million 30 za kumsaidia huyo mtoto wake sasa sijui niwape hawa vijana nilokuja nao huku au kama kuna uwezekano wa njia za bank niwatumie?" 

Kutokana na maendeleo ya kibank kutofika kijijini basi mwenyekiti aliomba kuongea na Haule na Joely kuwauliza kama wataweza kufikisha mzigo huo wa million 30 nyumbani hapo Haule na Joely walitabasamu moyoni na kumwambia mwenyekiti kua aondoe shaka hela itafika.

***
Mwenyekiti alikuja kwa bi Martha na kumueleza kuhusiana na mzigo utakaoingia hapo nyumbani mda sio mrefu wote walishangilia hadi Denis alifuarah kuona kua hataishi tena maisha ya uyatima maana analetewa rambirambi ya kumtunza na kumpatia elimu bora.

***

Ndani ya saa mbili na nusu makamanda wa Filbet walikua getini wakiwa wamejipanga kikamilifu ambao wao hutembea na silaha zote hatari ikiwemo mabomu ya kurusha kwa mkono, sindano za sumu, bastola, visu nakadhalika ila pale ukutanapo nao huwa wamevaa suti na begi ya kuning'iniza na biblia kwa hiyo wanapopita katikati ya watu salamu ya Bwana Yesu Asifiwe hutawala na pale wanapopanda daladala huachiwa siti. 

Haule na Joely waliachwa ndani na Filbet alitoka nje kuongea na makamanda wake na kuwapa ramani na picha za watu wanaostahili kufa ambapo kwa wakati huo aliwapa picha ya bi Martha pekee maana tayari Haule na Joely wameonekana ndani, kwa bahati nzur picha ya Denis haikupatikana kwa kua muda Filbet anachukua mkanda wa video Denis alikua hospital ila aliwaagizia sura yake nao kwa kutumia akili zao wakaunda taswira na kupata sura ya Dennis.

Baada ya makamanda kuchukua sura za wote basi wakamwondolea boss wao shaka kua kazi rahis sana na wataifanya kikamilifu.

***

Dennis alimuomba bibi yake kuelezwa historia ya baba ake bibi alishangaa sana maswali ya mjukuu wake huyo ila alianza kumuelezea ingawa aliamini atamharibu kisaikolojia 

"Mjukuu wangu baba yako alikua mtoto wangu wa mwisho kati ya 6 ila yeye alikua na roho ya kinyama sana maana aliwauwa ndugu zake wote kwa kuwachanganyia  sumu kwenye chakula ili tu amiliki ardhi na mifugo yao pia mbaya zaidi ni pale alipomuua baba yake yaani mume wangu kwa kumkatakata mapanga hivyo alifanikiwa kuteka vitu vyote na kuviuza na tokea mama yako aage dunia basi yeye analetwa jana hapa nyumban". 

Bi Martha alishindwa kuendelea maana aliingiwa na huruma kumweleza mjukuu wake mambo yalomzidi umri hadi uzito.

***

Baada makamanda wa Filbet kupata ramani ya kila kitu walienda kupunzika kwa kujiandaa na kazi ambayo itafanyika kesho yake ikiwa ni siku pia ya kuanua tanga ndo ilipangwa Haule Joely wasafirishe pesa.

***

Giza liliingia Dennis akaingia ndani na kujifungia huku akilia kwa uchungu mambo bibi ake aliyomuelezea yalimfanya aone kama yeye ndo atakayerithi dhambi za baba yake hapo akakata tamaa ya kuishi.

***
Haule na Joely walikesha macho wakiuwaza msemo , (mtoto wa mwenzako sio wako) wakisubiri pakuche.

Je nini kitatokea ? tukutane tena Alhamisi panapo majaliwa.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: