Saturday, September 2, 2017

Maafa ya Houston uokozi unaendelea

ad300
Advertisement
Shughuli za kuokoa majeruhi kufuatia dhoruba ya kitropiki ya kimbunga iliyotokea na kupewa jina Harvey, mjini Houston Marekani zinaendelea.
 
Kulingana na Mshauri wa masuala ya usalama wa Rais Donald Trump, Tom Bossert, alisema kwamba takriban watu 1,000 wameathiriwa vibaya na balaa hilo.

"Ikulu ya Marekani itawasilisha ombi la dharura katika bunge la Congress kuomba fedha za ziada ili kuweza kukabiliana na tokio hilo," alisema kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Rais Trump mpaka sasa amechangia kiasi cha dola milioni moja kutoka kwenye mapato yake binafsi ili kusaidia waathirika.

Hata hivyo ameutembelea mji wa Rockport, ulioko Texas ili kutathmini hali ilivyo.

"Serikali iko pamoja na kila mtu aliyeathirika wakati wote," alisema makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence baada ya kuzuru eneo la maafa hayo.

Taarifa zinasema nje ya mji wa Houston, moto unaendelea kuwaka kwenye kiwanda kimoja cha kemikali, kilichozungukwa na maji pande zote kufuatia mafuriko hayo..

Shirika la Ulinzi wa Mazingira la Marekani limehakikisha kwamba hakuna kemikali za sumu katika moshi unaoenea eneo hilo.
Hadi kufikia sasa, vyombo vya habari vya nchibi Marekani vimesema watu 30 ndio wameripotiwa kupoteza maisha kwa maafa hayo ya kiasili.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: