Wednesday, August 30, 2017

Yanayoendelea kesi ya NASA kupinga ushindi wa Rais Kenyatta

ad300
Advertisement
Siku ya tatu ya kusikiliza kesi ya kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta, imeisha kwa Wakili Pheroz Nowrojee anayemwakilisha aliyekuwa mgombea kiti cha Urais kwa Muungano wa NASA Raila Odinga kuvutana kwa hoja na vifungu vya sheria dhidi ya mwenzake anayemwakilisha Rais Kenyatta, Ahmednassir Abdullahi.

Wakili Abdullahi aliiomba Mahakama ya Juu ya nchi hiyo, ambayo ndiyo inasikiliza kesi hiyo chini ya majaji saba, itupilie mbali uchaguzi mkuu uliompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta kwa alichokidai kwamba mtandao wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ilidukuliwa ili kura hewa  zijumuishwe na kura halali hatua iliyompa ushindi Kenyatta.

Akiwasilisha malalamiko yao, mbele ya mahakam hiyo, wakili huyo alimtuhumu Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati na maofisa wenzake kuwa waliruhusu mifumo yao ya kupokea na kuhesabu kura ichezewe ili kura za mgombea wa Jubilee ziwe nyingi kuliko zile za NASA.

Baada ya hoja zake, Wakili Ahmednassir Abdullahi anayemwakilisha Rais Kenyatta aliiambia mahakama hiyo kuwa upande wa NASA ukiongozwa na wakili wao hauna ushahidi kwenye malalamiko yao na kwamba mahakama itupilie mbali shauri lao akiliita kuwa ni porojo tu. 

Kesi hiyo inasimamiwa na jopo la majaji saba ambao ni David Maraga, Philomena Mwilu, Mohammed Ibrahim, Jackton Ojwang, Njoki Ndung’u, Smokin Wanjala na Isaac Lenaola.

Majaji hao wana kibarua kigumu cha kuamua Ijumaa hii Setemba 1, ikiwa uchaguzi wa urais ulikuwa halali ama la.

Wakiongozwa na Jaji mkuu (CJ) David Maraga, majaji hao wamelazimika kusoma ushahidi uliwasilishwa katika nakala zaidi ya 70,000.

Suala kuu ambalo majaji hao waliliangalia kwa umakini ni kama tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC ilifuata sheria ilipoandaa uchaguzi huo wa Agosti 8, mwaka huu.
Uamuzi wa majaji hawa unasubiriwa kwa hamu ikitiliwa maanani Jaji Maraga alikuwa ametofautiana na uamuzi wa mahakama hiyo hiyo mwaka 2013 chini ya uongozi wa Jaji Willy Mutunga.
Majaji hao waliambiwa na Raila Odinga kwamba IEBC ilikiuka sheria na uamuzi wa mahakama ya rufani, kwa kuruhusu wasimamizi wa maeneo 290 ya uwakilishi bungeni watangaze moja kwa moja matokeo ya urais.

Wakati hayo yakiendelea, wafuasi wa Uhuru Kenyatta akiwemo Seneta Kithure Kindiki wa Tharaka Nithi, aliwataka wafuasi wote wa Jubilee kuwa imani na ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta juu ya uamuzi wao wa Agosti 8, mwaka huu.

Alisema wafuasi hao na wote wenye mapenzi na taifa hilo wanapaswa kuweka matumaini yao kwa Mungu kuwa ndiye mwenye uamuzi wa mwisho.

Mlifanya kazi yenu ipasavyo ya kupiga kura, mkaweka imani yenu kwa tume huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuwa ingejumlisha kura zenu kwa uadilifu na kwa sasa mmejipata katika taasisi yenu ya mahakama na ambayo uamuzi wake lazima uambatane na msingi wa sheria zlizopendekeza ndani ya katiba yenu ya kujiamulia hivyo ondoeni shaka kabisa,” alisema.
Pia aliongeza kuwa wafuasi wa Rais Kenyatta walianza mapema kuonyesha kuwa na mienendo ya kiimani, kuwa ni wacha Mungu na wamekuwa kwa njia ya uwazi wakifanya maombi yasiyo na unafiki kwa ajili ya kuliombea taifa la Kenya.

Ni maombi yaliyotufanya tushinde uchaguzi wa mwaka 2013 tukiwa katika mazingara magumu ya kutukwamisha lakini tukapata amani ambapo wengi wetu ndani ya siasa za Uhuru Kenyatta tulikuwa tumeathiriwa na ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007 na kesi za ICC zikatuumiza zaidi lakini kwa msaada wa Mungu tukavuka," alisema seneta huyo.
Aidha, alihitimisha:  "Ikiwa Mungu ndiye alipanga kuwa Rais Kenyatta ataongoza taifa hili katika kipindi cha 2017 hadi 2022, kama vile alivyopanga ataongoza 2013 hadi 2017, hakuna la kuhofia kwa kuwa hata uamuzi uende upande gani, hoja kuu ni kuwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu yatakuwa yametimia."




Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: