Thursday, August 17, 2017

Watoto mapacha walioungana wafariki Muhimbili

ad300
Advertisement
Watoto mapacha walioungana na ambao walikuwa wamelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam, wamefariki dunia.

Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa Hospitali hiyo, Neema Mwangomo, pacha hao waliokuwa wakifanyiwa vipimo ili kuwaanda kwa upasuaji hivi karibuni, walifariki Jumanne wiki hii hospitalini hapo.

Neema alisema watoto hao walizaliwa wilayani Kilosa mkoani Morogoro katika kijiji cha Chaumbele.

Watoto hao walioshikana chini ya kifua na tumboni walikuwa wakitumia ini moja na mishipa ya moyo lakini kila mmoja alikuwa na tumbo lake.

Awali, daktari wa watoto hospitalini hapo, Dk. Zaituni Bokhary, alisema kwamba pacha hao wangeweza kutenganishwa wakifika umri wa miaka 6 tofauti na walivyokuwa walipofikishwa hospitalini hapo.

Taarifa zaidi za kitaalamu juu ya habari hii imeelezwa na hospitali hiyo kuwa itatolewa hivi karibuni.

Mungu aziweke roho zao mahali pema peponi Amen.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: