Thursday, August 17, 2017

Rais aagiza raia kupimwa Ukimwi kwa lazima

ad300
Advertisement
Rais wa Zambia, Egdar Lungu, ametangaza kuwa ni lazima kwa raia wa nchi hiyo kupimwa virusi vya ukimwi na ukimwi ili kujua afya yake.

Amesema ugonjwa huo kwa miaka mingi sasa umeendelea kuwa janga kuu duniani huku kitendawili cha tiba yake kikikosa mteguzi.

"Ni kupitia maambukizi ya janga hili hatari duniani nalazimika kuagiza kila mmoja katika nchi hii apimwe iwapo ana virusi vya Ukimwi, si hiari," alisema.

Rais huyo alitoa kauli hiyo wiki hii nchini humo wakati wa uzinduzi wa Baraza la Ukimwi Lusaka, mji mkuu wa Zambia.

Alisema nchi ya Zambia imeorodheshwa na shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa kati ya nchi zenye viwango vya juu zaidi vya maambukizi ya Ukimwi Kusini mwa Bara la Afrika kwa asilimia 11.6.

"Kwa takwimu hizo, inaonekana watu walio na umri wa kati ya miaka 15 na 49, wanaishi na virusi vya Ukimwi hapa Zambia, hali hii inatisha," alisema.

Rais Lungu alisema tayari uamuzi alioutoa tayari ulizungumzwa kwenye baraza la mawaziri la nchi hiyo hivyo mtu kupimwa na kupewa ushauri wa matibabu si hiari katika jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa Ukimwi Zambia.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: