Sunday, August 20, 2017

Taarifa za usajili Uingereza

ad300
Advertisement
Wakati klabu mbalimbali barani ulaya zikikimbizana kuboresha vikosi vyao kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili, West Brom wamemnunua kiungo wa kati wa zamani wa England Gareth Barry kutoka Everton kwa bei ambayo haijafichuliwa. 

Mchezaji huyo wa miaka 36 amecheza mechi 628 katika Ligi ya Premier nchini Uingereza katika misimu 21 akichezea Aston Villa, Manchester City na Everton. 

Barry sasa anahitaji kucheza mechi tano zaidi ili kuvunja rekodi ya nyota wa Manchester United Ryan Giggs ya mechi 632. 

Wakati huo huo, mchezaji Gylfi Sigurdsson ameihama klabu ya Swansea na kujiunga na Everton. 

Nyota huyo kutoka Iceland, amesajiliwa kwa jumla ya pauni milioni 45 za Uingereza ambacho ndio kiwango cha juu kwahi kutumiwa na Everton kusajili mchezaji. 

Klabu ya machester city kwa upande mwingine bado wanawasaka wachezaji kadhaa kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo la usajili.
 Matajiri hao kutoka jiji la Manchester wanaoongozwa na Pep Guardiola sasa wanamtaka beki wa zamani wa Manchester United, Johny Evans anayesakata soka lake katika klabu ya West Brom ila klabu hiyo tayari imekataa pauni milioni 18 za Uingereza iliyotolewa na Man City.

Dirisha la usajili la majira ya joto linatarajiwa kufungwa rasmi Agosti 31, mwaka huu.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: