Sunday, August 20, 2017

Afrika yaambulia mmoja kuwania mchezaji bora FIFA

ad300
Advertisement
Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) limetangaza orodha ya majina ya wachezaji 24 wanaowania tuzo la mchezaji bora wa FIFA kwa mwaka huu. 

Limetoa orodha hiyo huku ikibainika kuwa klabu ya Real Madrid ya Hispania ndio imeingiza majina ya wachezaji wengi zaidi kuliko zingine. 

Wachezaji saba wa Real Madrid wamepata nafasi ya kuingia katika orodha hiyo, ambayo mchezaji mmoja pekee wa Afrika amefanikiwa kuteuliwa. 

Pierre Emerick Aubameyang ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Gabon anayechezea Borussia Dortmund ya Ujerumani ndiye mchezaji pekee aliyebahatika kuwemo kwenye orodha hiyo. 

Baadhi ya wachezaji kutoka ligi kuu ya Uingereza waliotajwa katika orodha hiyo ni Alexis Sanchez wa Arsenal, Harry Kane wa Totenham Hotspurs na Eden Hazard, N'Golo Kante wote kutoka Chelsea.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: