Monday, August 28, 2017

Serikali, Waasi watifuana

ad300
Advertisement
Watu 19 akiwemo mwandishi wa habari raia wa Marekani wameuawa katika mapigano mapya yaliyohusisha vikosi vya serikali na waasi wenye silaha katika Jimbo la Yei, nchini Sudan Kusini.

Msemaji wa Jeshi la nchi hiyo, Santo Domic Chol, jana aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa mapigano hayo yaliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita, yalianza baada ya kundi hilo la waasi kufanya jaribio la kuvamia kituo cha kijeshi cha Kaya.

Alisema waasi 15 wameuawa katika makabiliano hayo huku jeshi la nchi hiyo likipoteza askari wake watatu waliokuwa mstari wa mbele kwenye tukio hilo la kujibizana risasi.

Kuhusu mwanahabari wa Marekani, alisema mwandishi huyo ametambuliwa kwa jina la Christopher Allen, ambaye alikuwa akifanyia kazi na mashirika kadhaa ya habari nchini humo.

Sudan Kusini ilitumbukia katika machafuko na mapigano kati ya askari watiifu kwa Rais Salva Kiir na makamu wake wa zamani Riek Machar tangu mwaka 2013.

Vita vya ndani katika nchi hiyo changa zaidi barani Afrika vimewalazimisha raia takriban milioni tatu kuwa wakimbizi katika nchi jirani na wengine maelfu kuuawa.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: