Monday, August 28, 2017

Korea yajaribu matatu

ad300
Advertisement
Serikali ya Korea Kaskazini imerusha makombora yake matatu kwenye bahari iliyoko mashariki ya peninsula ya Korea kutoka Gangwon-do.

Taarifa zilizothibitishwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo vilisema jaribio hilo ni la kawaida kwenye mfululizo wa majaribio ya makombora ya balistiki ya nchi hiyo kwenye Peninsula ya Korea.

Ikulu ya Marekani ilisema jana kuwa Rais Donald Trump baada ya tukio hilo alisema anaendelea kufuatilia suala hilo kwa ukaribu kisha atachukua hatua.

Kwa upande wao Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ilitoa taarifa ikipinga kitendo hicho cha Korea Kaskazini, ambacho kimekwenda kinyume na maazimio ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Taarifa hiyo ilisema Pyongyang inatishia usalama wa kikanda na kimataifa, na kwamba Ufaransa inatoa wito kuitaka Korea Kaskazini kutekeleza majukumu ya kimataifa na kuachana na silaha za nyuklia.

Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya kimataifa ya baraza la juu la bunge la Russia, Konstantin Kosachev, alisema kitendo hicho cha Korea Kaskazini kimevuruga utatuzi wa suala la peninsula ya Korea na huenda kikaleta matatizo kwa nchi hiyo.
Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 comments: