Advertisement |
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,
amesema waandishi wa umma katika kata mbalimbali za jiji la Arusha na gharama
kubwa za upimaji wa ardhi ni baadhi ya sababu za migogoro mingi ya ardhi inawafanya wasio na uwezo kushindwa kumiliki ardhi.
Aidha aliwanyooshea kidole wanasiasa
pamoja na watendaji wa kata kwakua sehemu ya migogoro hiyo kwa maslahi yao
binafsi ya kisiasa badala ya kujali maslahi ya wananchi wanaowaongoza katika maeneo
yao.
RC Gambo alisema watu hao wamekuwa wakipenda
pesa zaidi kuliko kusimamia utu na haki za wananchi ambapo aliagiza kila
halmashauri za mkoa wa Arusha kuhakikisha wanaweka taarifa za walalamikaji
wa migogoro ya ardhi ili malalamiko hayo yashughulikiwe na kupatiwa
ufumbuzi.
Aliyasema hayo leo Agosti 29, kwenye kikao chake na wataalamu wa Ardhi,Viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU), Idara ya Uhamiaji, Polisi, Watendaji wa Kata na
wananchi wenye kero mbalimbali za ardhi jijini Arusha ili kuzisikiliza na
kuzitatua.
Katika kikao hicho kilichofanyika katika
ofisi za jiji la Arusha, alisema migogoro mingi ya ardhi inasababishwa na
gharama kubwa za upimaji ardhi ambazo wananchi hawazimudu jambo ambalo alisema
linapaswa kuangaliwa upya na kuweka gharama rafiki kwa wananchi
na kuwawezesha kumiliki ardhi.
Pia alionya wanasiasa kuacha mara
moja tabia ya kutumia kero za wananchi kama mtaji wao wa kisiasa kwakua
kwakufanya hivyo hawaijengi jamii wanayoingoza Katika kuzipatia ufumbuzi kero
zao bali malumbano yasiyo na tija.
Akizungumzia watendaji wa kata,
alisema wapo katika kata hizo kwaajili ya kusogeza huduma bora za kiserikali
kwa wananchi na pale kero inapowashinda wanapaswa kuiwasilisha ngazi za juu yao
badala ya kuitumia migogoro hiyo kujipatia fedha huku migogoro
ikiendeleakuwatafuna wananchi.
Kuhusu waandishi wa umma aliwataka
kuwaandikia wananchi mikataba isiyo na utata kwa lengo la kujali fedha zaidi
kwani baada ya wao kupata fedha zao kinachofuata ni kuwaaachia wananchi
waliouziana maeneo migogoro isiyokwisha.
Aidha alikemea tabia ya nakala za
hukumu za mashauri ya ardhi kucheleweshwa kutolewa halia mbyo inasababisha wale
wananchi wanyonge ambo wameshinda katika kesi zao kukosa ushahidi na kuzidiwa
nguvu na wale wenye fedha na ardhi zao kuchukuliwa.
Hili suala ni lazima sasa tulichukue kwa uzito wa pekee haiwezekani watu wanakero za ardhi tangu mwaka 1989 hadi leo hii inamaana hakuna viongozi wanaoshughulikia suala hili, inasikitisha hapa kunarushwa ndani yake, kwanini watu walalamikie mipaka au njia kwa njia sasa ni lazima tujipange kuhakikisha changamoto hii inaisha," alisema.
Awali baadhi ya wananchi wenye kero
hizo, Rose Livingstone Mkazi wa Sekei alisema amehangaika na kesi yake ya ardhi
tangu mwaka 1989 hadi leo hii na hajapewa nakala za hukumu sita ambapo hadi
sasa amepata nakala moja tu ya hukumu na ameambiwa atoe sh. milioni
7.
Mimi sina hiyo sh. milioni 7 na hadi sasa nahangaishwa kuhusu eneo langu lakini mtu ninayepambana naye anauwezo sina jinsi lakini mahakama imetoa amri abomolewe ukuta ule sasa mimi naombeni mnisaidie kuhusu haki yangu," alisema.
Kutokana na hilo, Gambo aliamuru mhusika huyo abomolewe ukuta huo ili mlalamikaji
apewe eneo lake pia alitoa rai kwa wananchi wanaotaka kupimiwa ardhi kuungana
kwa pamoja kwenye mitaa yao ili waweze kugharamia upimaji wa maeneo yao kwa sh.
milioni 1 zitakazowapatia hati miliki za ardhi.
0 comments: